Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu), Dkt Jim Yonazi amekipongeza Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA) kwa kuanzisha kozi nzuri zinazoendana na mahitaji ya soko kwa sasa.
Dkt. Yonazi ameyasema hayo alipotembelea banda la IAA katika maonesho ya 48 ya biashara baada ya kuelezwa kuhusu kozi mbalimbali zinazotolewa na Chuo, ikiwemo shahada ya Usalama wa Mtandao (cyber security) na shahada ya Ukaguzi wa Hesabu (Audit and Assuarance).
Pia, ameipongeza IAA kwa kukamilisha ujenzi wa Kampasi yake ya Dodoma baada ya kupokea maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Chuo, Bw. Anorld Kavishe, kuwa ujenzi umekamilika na ifikapo Oktoba 2024 Kampasi itahamia Njedengwa.
Chuo cha Uhasibu Arusha kinaendelea kuwakaribisha Wananchi kutembelea Banda lake ambalo liko katika Jengo la Wizara ya Fedha katika maonesho ya 48 ya Biashara maarufu kama Sabasaba.
Post A Comment: