Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Bi. Rose Robert Manumba ameongoza timu ya Wataalam kutoka Halmashauri kusikiliza na kujibu Kero za Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Njiwa.
Kero mbalimbali zilizoibuliwa na Wakazi wa njiwa ni pamoja na kutaka ufafanuzi wa huduma za afya,
Migogoro mbalimbali ya ardhi kati ya vijiji, taasisi na mtu mmoja mmoja,Stakabadhi ghalani, hatma ya vitongoji halali vilivyopo maeneo ya hifadhi,Migogoro ya wakulima na wafugaji.
Baadhi ya kero hizo zilipatiwa majibu ya hapo kwa hapo na Mkurugenzi pamoja na Wataalam kutoka Halmashauri na nyingine Mkurugenzi Aliahidi kuwasilana na Tasisi husika na atawarejea Wananchi kwa majibu ndani ya muda mfupi.
"Niwahakikishie Wananchi wa Njiwa yale yote niliyoyachukua kwaajili ya utekelezaji nitaenda kuyasimamia ipasavyo,kuna yale ambayo nimeyatolea muda kwaajili ya utekelezaji nitatimiza ahadi yangu, na hata yale ambayo sikuyatolea muda niwahakikishie kwamba naenda kufanya ufuatiliaji wa kina kuhakikisha kwamba yanatekelezwa ili kuondoa kero na changamoto zote zinazowakabili na kuhakikisha ufumbuzi unapatikana" amesema Mkurugenzi Manumba
Aidha Mkurugenzi amewataka Watumishi katika Kata ya Njiwa kutekeleze majukumu yao kwa uaminifu na uadilifu, kuzingatia kanuni na miongozo yote inayowataka kutekeleze majukumu yao kikamilifu kama Watumishi.
Hata hivyo, Mkurugenzi Manumba amewashukuru Wananchi wa Kata ya Njiwa kwa kushiriki kwa wingi katika mkutano huo na kuainisha changamoto mbalimbali zinazo wakabili na amewaomba Wananchi hao kuendelea kushirikiana na kutoa taarifa mbalimbali katika Ofisi ya Mkurugenzi.
Post A Comment: