Wananchi waishio Dar es Salaam, ambao ni wazaliwa wa Wilaya ya Makete, jana Juni 30,2024, wamepata Fursa ya kusomewa taarifa ya Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo ambayo imekuwa ikifanyika katika Wilaya hiyo.
Akisoma taarifa hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Ndg. William M. Makufwe, amesema kuwa Serikali imeboresha Miundombinu ya Elimu , Afya, Usafiri na Maji ili kuhakikisha Jamii inapata huduma iliyo bora, tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Aidha, Ndg. Makufwe amebainisha kuwa, Serikali imeongeza Bajeti ya Maendeleo katika Wilayani hiyo kutoka Bilioni 26 hadi 36, Ili kuhakikisha kuwa Wilaya hiyo, inaboreshwa katika utolewaji wa huduma za kijamii pamoja na kunyanyua uchumi wa Wilaya hiyo.
Sambamba na hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Makete, amewaomba wanamakete kuchangia Maendeleo Wilayani humo, kutokana na kuwepo fursa nyingi za kiuchumi zilizopo katika Wilaya hiyo, katika Kilim, Uvuvi, na Viwanda.
Kwa Upande wake, katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Ndg. Antony Sanga, amewashukuru Wanamakete kwa kutoa michango chanya katika Mkutano huo ambayo Umelenga kuikuza Makete kiuchumi, pamoja na kuhakikisha kuwa wahitimu wa vyuo vikuu wanatengenezewa uwezo wa kuajiriwa na kujiajiri.
Naye, Mbunge wa Makete, Mhe. Festo Sanga, amewataka Wanamakete kuungana na kuwa kitu kimoja katika kuwekeza Nyumbani, kwakuwa Makete ni Moja na Tuijenge Pamoja.
Sambamba na hayo, Mwenyekiti wa Chama Cha Maendeleo Wilayani Makete, MDA, Ndg. Clement Sanga, amewataka Wanamakete kuwaheshimu viongozi wa Wilaya ya Makete, pamoja na kushirikiana kiuchumi katika kuikuza Wilaya hiyo.
Akihitimisha Mkutano huo, Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka, Mkuu wa Wilaya Makete, Mhe. Juma Sweda, amesema kuwa, lazima kuwepo na mwendelezo wa Mikutano kama hiyo ili kuhakikisha kuwa Kila mtu anawajibika pamoja na kuweka maeneo ya Ushirikiano kimaendeleo.
Post A Comment: