Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Karatu Ndg.Juma Hokororo amekemea uzembe wa muhandisi, mafundi pamoja na wasimamizi wazembe wa miradi inayotekelezwa katika kituo cha afya buger baada ya kusuasua kwa miradi hiyo.
Mkurugenzi ametoa maelekezo hayo akizungumza na wakuu wa idara katika eneo la kituo hicho alipofika kukagua utekelezaji wa miradi hiyo ambayo ni jengo la mama na mtoto, vyoo matundu matatu, kichomea taka pamoja na mnara wa tenki.
Ambapo akikagua miradi hiyo amebaini kuwa uzembe mkubwa unafanyika katika jengo la mama na mtoto ambalo lilitakiwa kukamilika mapema lakini mpka sasa lionekana kutofikia hatua ya kuridhisha.
Amemuelekeza Mhandisi wa halamshauri pamoja na Msimamizi wa mradi huo kuhakikisha wanamtafuta fundi mwingine haraka ili kukamilisha mradi huo kwa ubora na kwa wakati.
Miradi hiyo inayotekelezwa katika kituo hicho cha afya ni fedha kutoka mradi wa miundombinu ya maji SWASH pamoja na fedha za ndani kutoka halmashauri ambapo ni zaidi ya milion 250 za kitanzania.
Post A Comment: