Mwenyekiti wa Kitongoji cha Magamba Kata ya Magamba wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga,Mahamudu Kikoti ameiomba serikali kuchukua hatua juu ya diwani anayedaiwa kunyanyaswa wananchi Kwa kuwapora mali zao Kwa mabavu,jambo ambalo  limepelekea wananchi kuishi kwa wasiwasi mkubwa.


Kikoti ameyasema hayo  wakati akizungumza na waandishi wa habari na kumwomba Mkuu wa Wilaya ya Lushoto,Japhari Mghamba kumchukulia hatua diwani wa Kata hiyo,Mathew Mbaruku anayetuhumiwa kunyanyasa wananchi wilayani hapo.


Amesema diwani huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto amekuwa akikabiliwa na tuhuma kadhaa  za kuwanyanyasa wananchi ikiwemo kujihusisha na vitendo vya kupora mali za wananchi, kubambikia kesi, na kuunda vikundi vya watu kwa ajili ya matukio ya kiuharifu.


"Hali hii inaleta wasiwasi mkubwa kwa wananchi wa Kata ya Magamba.Ni muhimu vyombo vya sheria vichukue hatua mara moja ili kuhakikisha usalama na haki kwa wananchi wote.Kwa kushirikiana, tunaweza kufanya kazi kuhakikisha kuwa watu wanapatikana na haki inatendeka".


Mwenyekiti huyo  amemuomba Mkuu wa Wilaya hiyo,ambaye hana muda mrefu tangu ateuliwe na Mhe Rais Mnamo Machi 12 Mwaka huu  kwamba ni muhimu kusimamia usalama na haki za wananchi na  kwa kushirikiana naye,wanaweza kuleta maendeleo makubwa katika  kufanikisha lengo la kukuza uchumi wa wilaya na taifa kwa pamoja.


"Hivyo tunatumia fursa hii kukuomba umchunguze diwani Mathew Paul,usimwamini sana,amekuwa mwiba kwa wananchi  na kujificha kwenye mgongo wa serikali hapa wilayani.Ninavyokwambia ameweka vijana Katika Kata ya  Magamba Kuhakikisha taarifa za kila Mgeni atakayefika anazipata,na wasipo  jiridhisha  na mazungumzo yao basi hicho kikundi kinafanya matukio ya kiuharifu Kwa Wananchi"


Kikoti ameongeza Kwa kusema  "Mimi kama  Mwenyekiti wa kitongoji hali hii inanipa wakati mgumu sana kiutendaji maana alishawahi kunidhuru Kwa kuwatuma watu kunikata mapanga kwa nia ya kutaka kupoteza  maisha yangu lakini jeshi la police limenisaidia".


Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo amesema hivi serikali ilituma watafiti kwenda kukusanya taarifa eneo la uchimbaji madini ambalo awali Waziri Mkuu alisitisha shughuli za uchimbaji mpaka pale watakapojiridhisha  kwamba madini hayo hayana madhara kwa wanadamu ambapo walishangazwa kufanyiwa vurugu na genge linalomilikiwa na diwani huyo.


"Wakati tupo kwenye eneo la mgodi huo genge likajitokeza na kutaka  Kutudhuru Kwa  mapanga,hali ambayo  iliwapa wasiwasi watafiti hao,tukarudi kwako ukatupatia  ulinzi tunashukuru  kazi  imefinyika  Salama" amesema Mwenyekiti huyo.

Mjumbe wa Serikali ya Kijiji hicho,Twaha Waziri Mkuzu amemwomba Mkuu wa Wilaya aingilie kati kwani diwani huyo amekuwa akiwatishia maisha,kutowapa ushirikiano pia kutumia mabavu kurudisha maendeleo ya wilaya hiyo nyuma kwani viongozi wa Serikali ya kijiji  wamekuwa wakifanya  kazi chini ya maelekezo yake.


"Ametunyanyasa sana hasa viongozi wa Serikali ya Kijiji kipindi ambacho DC aliyetanguliwa alikuwepo na tuna ushaidi wa hiki tunachokisema kuhusu  Mhe. kubecha.Sasa tunaona uwepo wako wewe hapa,Lushoto imeanza kubadilika ila kuna mwiba mzito hapo Katika Halmashauri yako ni kiongozi wa Halmashauri Mhe Mathew Paul anatumia mabavu kurudisha maendeleo nyuma" amesema Mkuzu.


Akizungumza kuhusu malalamiko hayo,Mkuu wa Wilaya ya Kushoto,Japhari Mghamba amesema bado  yupo kwenye ziara za kusikiliza Kero na kutatua migogoro ya Wananchi ambapo  ameahidi  kufika hivi karibuni katika Kata hiyo  kuwasikiliza Wananchi ambapo amewataka wananchi kuondoa  wasiwas kwani jukumu lake ni  kuhakikisha wanaishi salama na kufanya majukumu yao ya kila siku bila bugudha.


Akijibu tuhuma hizo Kwa njia ya simu,Diwani wa Kata ya  Magamba,Mathew Mbaruku amesema hana majibu ya tuhuma hizo na kuuliza "wewe nani alikwambia" Kisha kukata simu mara moja na hata alipopigiwa mara kadhaa hakupokea simu aliyopigiwa na mwandishi wetu.


 



Share To:

ASHRACK

Post A Comment: