Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Musoma Mjini Mkoani Mara, kimekabidhi mifuko ya Saruji 138 kwaajili ya Ujenzi wa jengo la uchumi wa Chama cha Mapinduzi (Ukumbi)Mkoa wa mara, ambapo uje wa jengo hilo umefikia Asilimia 45 huku kukamilika kwake likihitaji zaidi ya shilingi Milioni 700.
Akizungumza wakati wakukabidhi mifuko hiyo ya Saruji mwenyekiti wa CCM wilaya ya Musoma mjini alisema kukabidhi mifuko hiyo niutekelezaji wa maagizo ya Halmashauri kuu ya Mkoa kuhakikisha wanakabidhi Saruji kwaajili ya Ujenzi wa jengo hilo.
"Tulipokea maelekezo kutoka Mkoani kwa maana ya halmshauri juu ya mkoa ikitutaka Chama Wilaya zote kuchangia kitega uchumi hicho Sisi Musoma mjini tunakabidhi mifuko ya Saruji 138 ambayo itaenda kuongeza nguvu katika utekelezaji wa mradi huo"Alisema Benedictor Magiri Mwenyekiti wa CCM Musoma Mjini.
Akipokea msaada huo katibu wa CCM Mkoa wa Mara Ibrahim Mjanakheri amesema ujenzi wa kitega uchumi hicho cha Chama cha Mapinduzi Mkoani mara kimefikia Asilimia 45 huku hadi kukamilika likikdiliwa kutumia kiasi cha shilingi Milioni 700.
"Tumepokea mifuko ya saruji 138 na wamenihakikishia kuna mifuko mingine inakuja baada ya hii mchango wao unatusaidi kutoka kwenye mifuko 800 ambayo tunakusudia itatumika kwenye shughuli mbalimbali zinazoendelea na mchango hii imesaidia kazi inaendelea tunawaomba wadau wendelee kutuchangia jengo letu likikamilika litakuwa na uwezo wa kubeba watu kwa pamoja 2300"Alisema Ibarahim Mjanakheri katibu wa CCM Mkoa wa Mara.
Mjankkheri amesema kukamilika kwa jengo hilo kutasaidia kuongeza Mapato kwa Chama.
Post A Comment: