MADEREVA bodaboda zaidi ya 200 katika Wilaya ya Tanga mkoani Tanga.wamehitimu Mafunzo ya usalama barabarani yaliyokuwa yakitolewa na Shirika la Amend kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.


Katika Mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Ubalozi wa Uswiss nchini Tanzania yamehusisha matumizi sahihi ya barabara, sheria za usalama barabarani, umuhimu wa utoaji huduma ya kwanza kwa majeruhi pamoja na mafunzo kwa vitendo.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Mkoa wa Tanga ACP Bernard Zacharia amesema aodaboda wamekua sehemu kubwa ya urahisishaji usafirishaji kwa abiria na mali zao,hivyo mafunzo waliyoyapata madereva bodaboda hao wa Wilaya ya Tanga na maeneo mengine ya mkoa huo yatawasaidia wao na abiria wao kuwa salama.

Amesema kwa Wilaya ya Tanga madereva bodaboda maarufu maofisa usafirishaji 204 wamehitimu mafunzo ya msasa ya usalama barabarani na kusisitiza waliopatiwa mafunzo wahakikishie wanakuwa.mabalozi kwa madereva wengine.

Akizungumza na madereva hao ACP Bernard Zacharia jeshi la police mkoa wa Tanga aliwaeleza - “bodaboda wamekua sehemu kubwa ya urahisishaji usafirishaji kwa abilia na mali zao. Mafunzo mlio yapata yatawasaidia sana ninyi na abilia wenu na wote kuwa salama

"Tunatarajia bodaboda Mkoa wa Tanga mtakua mfano wa kuigwa na mtakuwa mabalozi wazuri.Jeshi la Polisi linawahimiza kutii sheria bila shuruti na tunawashukuru Ubalozi wa Uswiss na Amend kwa ushirikiano huu na Jeshi la polisi kwa kuwaangalia vijana kwa ukaribu huu."

Kwa upande wake Mratibu wa Shirika la Amend Ramadhan Nyanza amesema wanaishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushirikiana kwa karibu na mashirika yasio ya kiserikali kuzifikia jamii.

Amesema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja kwa ufadhili wa Ubalozi wa Uswiss nchini Tanzania ,- Shirika la Amend kwa kushirikiana na wadau mbalimbali limefanikiwa kutoa mafunzo kwa vijana zaidi ya 900 kwa mkoa wa Dodoma na Tanga.

Pia amesema wanahimiza vijana kutumia fursa za mafunzo kama hayo ya usalama barabarani zikitokea wajitokeze kwani ajali za barabarani zinaepukika na wanaweza kuwasaidia wenzao wanapopata ajali ili kuendelea kuokoa maisha na kupunguza ulemavu wa kudumu.

"Mafunzo ya usalama barabarani tunayatoa bure kwa vijana hivyo tunaomba waendelee kujitokeza wanaposikia fursa hizi kwani zinasaidia kuengeza pato lao binafsi na pato la taifa kwa ujumla kama maafisa usafirishaji."








Share To:

Post A Comment: