Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Comrade Daudi Yassin ametumia mkutano wa hadhara wa wananchi wa Kijiji cha Ikokoto Wilayani Kilolo kusikiliza kero na na kuzitafutia majibu.
Mwenyekiti wa  CCM Mkoa wa Iringa Comrade Daudi Yassin ametumia mkutano wa hadhara wa wananchi wa Kijiji cha Ikokoto Wilayani Kilolo kusikiliza kero na na kuzitafutia majibu.

Na Fredy Mgunda, Iringa.

Mwenyekiti wa  CCM Mkoa wa Iringa Comrade Daudi Yassin ametumia mkutano wa hadhara wa wananchi wa Kijiji cha Ikokoto Wilayani Kilolo kusikiliza kero na na kuzitafutia majibu.

Miongoni mwa kero walizolalamikia wananchi hao ni ubovu wa barabara, umeme kwa baadhi ya vitongoji, maji, jengo la kupumzikia wagonjwa zahanati ya kijiji na hosteli shule ya Sekondari Ilula wanakosoma watoto wao.

'Mwenyekiti Yassin'ametumia ziara yake aliyoifanya Jana Juni 12, 2024 kuzitafutia majibu kero hizo kutoka kwa wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo. 

Kwenye kero ya Umeme, wananchi wakiomba kupunguziwa bei kubwa ya kuunganishiwa umeme ombi ambalo kiongozi wa Tanesco Wilaya ya Kilolo alipowasiliana na makao makuu ya REA ombi Hilo lilipokelewa na kuahidiwa bei itapungua.

Kutokana na majibu ya viongozi wa Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, wakazi wa Ikokoto waliahidi kuendelea kumuunga mkono Dk Samia Suluhu Hassan.

Hata hivyo walishukuru uwepo wa maendeleo kwenye kijiji chao ambacho licha ya kuwepo Mlimani, huduma za kijamii nimefika ikiwemo zahanati.

Mwenyekiti Yassin alisema wananchi hao wasiwe na wasiwasi kwa sababu atafuatilia na kuhakikisha majibu ya wataalamu wa Serikali yanafanyiwa kazi.

"Nimekuja kuwasikiliza nanyi mmeeleza kero zenu ambazo tumepata majibu, Serikali ya awamu ya sita ya Dk Samia Suluhu Hassan ni ya wananchi na sikivu, kazi yetu ni kuwasikiliza," amesema Yassin.

Kero zote walizotoa wataalamu hao zitaanza kutatuliwa katika bajeti ya Serikali ya mwaka 2024/25.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: