Afisa Tarafa ya Idodi, Makala Mapesah J.J akiongea na wananchi juu ya malezi na makuzi ya watoto ili kujenga taifa lenye watu imara
Afisa Tarafa ya Idodi, Makala Mapesah J.J akiongea na wananchi juu ya malezi na makuzi ya watoto ili kujenga taifa lenye watu imara
Na Fredy Mgunda, Iringa.
WAZAZI na Walezi wa Kijiji cha Tungamalenga Tarafa ya Idodi Wilaya ya Iringa Mkoani Iringa wametakiwa kuacha Tabia ya ulevi na kutotekeleza majukumu yao ya malezi kwa watoto ili kuhakikisha uliinzi na usalama wa watoto wao.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji hicho Afisa Tarafa ya Idodi, Makala Mapesah J.J alisema kuwa kumekuwa na ongezeko la vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto wa kijiji cha Tungamalenga.
Mapessah alisema kuwa matukio ya ukatili kwa watoto katika Kijiji hicho yanachangiwa na wazazi na walezi kutumia muda mwingi kwenye kilimo cha Mpunga na Kuwaacha Watoto kwenye mazingira hatarishi kwa usalama Wao.
Alisema kuwa tatizo la Ulevi kwa wazazi na walezi Linatajwa Kuchangia Watoto Kutelekezwa na kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo kwa kiasi kikumbwa vitendo hivyo huishia ngazi ya familia.
Mapessah alisema kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia vinatakiwa kutolewa taarifa kwa mamlaka zinazohusika ili kukomesha kabisa vitendo hivyo.
Alimalizia kwa kusema Kuwa Mkakati wa Serikali ya Tarafa na Kijiji cha Tungamalenga ni kuendelea kutoa elimu ya Malezi, Makuzi, Ulinzi na Usalama kwa Watoto Wenyewe, Wazazi na Walezi Pamoja na Jamii kwa ujumla.
Watoto Wakisoma Risala yao Kwenye Maadhimisho hayo wameitaka jamii na hasa Wazazi kutopoka haki yao ya malezi na kuwaacha wakijilea wenyewe huku pia wakitaka hatua za kisheria kuchukuliwa kwa wanaotenda ukatili.
Post A Comment: