na Dickson Mnzava, Same.

Wananchi wa Tarafa ya Mamba Vunta iliyopo katika Jimbo la Same mashariki wilayani Same Mkoani Kilimanjaro wametoa shukrani zao kwa serikali ya awamu ya sita inayongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Wamesema pongezi zinakuja baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Vituo viwili vya afya ndani ya tarafa hiyo pamoja na ujenzi wa barabara iliyowatesa kwakipindi kirefu wananchi hao barabara ya Hedaru Vunta Miamba.

Akizungumza kwenye kikao cha kusoma ilani ya Chama cha mapinduzi mbele ya viongozi wa Chama hicho ngazi ya ubalozi,mashina hadi uongozi wa Chama wilayani mbunge wa Jimbo la Same mashariki Anna kilango katika tarafa ya Mamba Vunta Kata ya Bwambo ameishukuru sana serikali kwakutekeleza miradi hiyo.

Kilango amesema kukamilika kwa ujenzi wa Vituo viwili vya afya ndani ya tarafa hiyo kutapunguza vifo hasa kwa Mama wajawazito ambao walikuwa waathirika wakubwa katika kupata huduma za Afya huku pia akisema uwepo wa Vituo hivyo sasa unaenda kuondoa adha kwa wananchi wote wa maeneo hayo.

"Hakika katika kipindi ambacho serikali imetupa fedha nyingi za miradi kwenye jimbo letu la Same mashariki ni kipindi hiki cha serikali ya awamu ya sita inayongozwa na Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan tumepokea fedha nyingi sana katika miradi ya elimu, Afya na miundombinu ya barabara"



"Alisema mbunge Anna kilango".
Mama Anna kilango amesema sambamba na hilo pia wananchi hao wanaishukuru serikali kwa kujenga barabara ya Hedaru Vunta Miamba ambayo imesaidia sana katika shughuli mbalimbali za maendeleo kwa wananchi wa maeneo hayo.

Amesema miongoni mwa miradi ambayo imepata fedha nyingi ndani ya Jimbo hilo la Same mashariki ni barabara akisema kwakiasi kikubwa sasa barabara za jimbo hilo zinapitika pamoja na ugumu wa jografia ya jimbo hilo.

Akitoa semina kwa viongozi hao wa CCM ngazi ya ubalozi na mashina Mwenyekiti wa CCM Wilayani Same Abdullah Suleiman Mnyambo amesema wameamua kutoa semina kwa viongozi hao ngazi ya Wilaya nzima lengo likiwa ni kuwajengea uwezo zaidi wa uelewa hususani kwenye kipindi hiki cha kuelekea kwenye chaguzi za serikali za mitaa pamoja na uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura.



Share To:

ASHRACK

Post A Comment: