Baadhi ya vijana wakiwa kwenye usahili wa kupata ajira za muda mfupi katika shamba la miti Sao Hill wilaya ya Mufindi mkoani Iringa 
Baadhi ya vijana wakiwa kwenye usahili wa kupata ajira za muda mfupi katika shamba la miti Sao Hill wilaya ya Mufindi mkoani Iringa 
Baadhi ya vijana wakiwa kwenye usahili wa kupata ajira za muda mfupi katika shamba la miti Sao Hill wilaya ya Mufindi mkoani Iringa 


Na Fredy Mgunda, Iringa 

Jumla ya vijana 192  kunufaika na ajira za ulinzi wa misitu ya shamba la miti Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kupitia ajira za muda mfupi.


Akizungumza wakati wa zoezi la usahili, Msaidizi wa Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Saohill Mhifadhi Mwandamizi Said Singano alisema kuwa kila mwaka shamba shamba la miti Sao Hill limekuwa na utaratibu wa kuajiri wafanyakazi kwa mkataba wa miezi sita kuanzia Julai mpaka Disemba kwa lengo la kuhakikisha misitu na maeneo yanayolizunguka shamba yanakuwa salama dhidi ya majanga ya moto.


Aidha Singano amewataka vijana wanaopata nafasi kufanya kazi kwa bidii na uadilifu na kufuata maelekezo wanayopewa na viongozi wao muda wote wanaokuwa kazini na kusisitiza kwa wale waliokosa nafasi kuendelea kushirikiana na shamba katika shuguli za ulinzi wa msitu kwani kuna kazi nyingi zinazoendelea ndani ya shamba.


Sambamba na hilo ametoa wito kwa wananchi wanaolizunguka shamba  kuendelea kuhakikisha wanafuata taratibu zilizowekwa za uanzishwaji wa moto ili kuepusha moto usiotarajiwa ikiwepo kuandaa mashamba kwa wakati, na kuacha kurina asali kwa kutumia moto.


Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha ulinzi wa msitu katika Shamba la Miti Saohill Mhifadhi Murya Sawa amesema kuwa zoezi la kukabiliana na majanga ya moto katika misitu ni jukumu la kila mwanachi hivyo linahitaji uzalendo na ukakamavu ili kukabiliana na hatari inayoweza kujitokeza na kuwataka wananchi wote kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya moto hatarishi.


Naye Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Mufindi Sajenti Ashery Kitundu amesema kuwa Jeshi la Zimamoto limekuwa likishirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kupitia Shamba la miti Saohill ili kuhakikisha kuwa elimu dhidi ya majanga ya moto hususani wa misituni inawafikia wananchi wengi Wilayani Mufindi ili kuhakikisha wanakuwa na tahadhiri dhidi ya moto hatarishi wa msituni.


Zoezi la usaili linatarajiwa kuendelea katika vituo vyote vya tarafa zote za Shamba Tarafa ya Kwanza Irundi, Tarafa ya Tatu Ihalimba pamoja na Tarafa ya Nne Mgololo.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: