Na Waf - Mpanda, Katavi


Kambi ya madaktari Bingwa wa Rais Samia katika Hospitali ya Halmashauri ya Mpanda imefanikiwa kumfanyia upasuaji na kutoa uvimbe kwenye kizazi Bi. Maria Wasira mwenye umri wa miaka 50 ulio msumbua kwa muda wa miaka 6

Akizungumza mara baada ya upasuaji huo Daktari wa Idara ya Upasuaji wa Hospitali hiyo Dkt. Baraka Kombe amesema mgonjwa huyo alikuwa anasumbuliwa na uvimbe katika kizazi kwa muda wa miaka 6, na kwamba halia ya upasuaji imeenda vizuri kwa kutoa uvimbe wenye uzito wa kilogram moja na mgonjwa yupo salama anaendelea vizuri.

"Kuna wagonjwa walikua wanaishi na magonjwa mbali mbali ambayo wengine walikua wamekata tamaa lakini ujio wa madaktari bingwa umefanya wameamka na kuja hospitali kutibiwa" Amesema Dkt Kombe

Nae Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Paulo Rugata amesema kupitia kampeni ya madaktari bingwa wa Rais Samia mpaka sasa wagonjwa zaidi ya 240 wamehudumiwa kwa muda wa siku tatu na kati yao 16 wamepangiwa kwa ajili ya upasuaji na wanted  kati yao wamesha fanyiwa upasuaji.  

"Kwa ushirikiano wa madaktari wetu na madaktari bingwa tuliopata wameweza kutujengea uwezo na kuona kazi kubwa zinaweza kufanyika na wagonjwa wakatoka salama bila tatizo lolote". Amesema

Bi. Magreth Abel Mkazi wa Mpanda Katavi kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya mpanda amemshukuru Rais Samia kwa kufanikisha uwepo wa Madaktari Bingwa katika wilaya hiyo  kwani huduma za kibingwa na bobezi zimesogea karibu zaidi na wananchi.

"Nimeonana na Madaktari bingwa wa Mama Samia, huduma zao zipo vizuri nawashukuru sana kwa kazi wanayoifanya nilikuwa nasumbuliwa na tumbo na mpaka sasa naendelea vizuri". Amesema Bi Magreth.

Kwa upande wake kiongozi wa Madaktari Bingwa wa Halmashauri ya Mpanda Dkt. Anna Asenga amewahimiza wananchi katika wilaya hiyo kuendelea kujitokeza kwa wingi kupata huduma za kibingwa na bobezi kwa muda uliobakia. 

"Sisi bado tupo tunatoa huduma mpaka Tarehe 14 June 2024 njoeni mpate huduma za kibingwa na bobezi na kwa atakaehitaji  upasuaji atafanyiwa hapa hapa hospitali ya wilaya Mpanda Dc" amesema Dkt. Asenga







Share To:

Post A Comment: