Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM),Mkoa wa Geita ,Manjale Magombe , amemuhakikishia ushindi Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Rehema Sombi kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa,vijiji pamoja na vitongoji  ni kutokana na  hatua kubwa za kimaendeleo ambazo zimefanywa na Rais Samia Suluhu Hassan .

Manjale ameyasema hayo  wakati wa shughuli za ufunguzi wa kambi za mafunzo kwa vijana wa CCM ambayo yanafanyika kwenye Kata ya Namonge Wilayani Bukombe Mkoani Geita.

Amesema wanaamini wanaenda kwenye uchaguzu mkuu wa serikali za mitaa,vijiji na vitongoji wakiwa na imani kwamba hakuna ambacho watapoteza kutokana na hatua kubwa za kimaendeleo ambazo tayari zimekwisha kufanywa kwenye maeneo mbalimbali yaliyomo ndani ya mkoa wa Geita.

“Leo Mhe Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa utazindua kambi rasmi ya mafunzo kwa vijana wa CCM,mafunzo ambayo yamelenga kuwafundisha vijana kuijua historia ya Chama,Lakini pia watajifunza maadili mema ya uongozi ndani ya chama tunataka tunapokwenda kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa wawe wameiva kwaajili ya kwenda kunadi sera za chama chetu pamoja na utekelezaji wa Ilani”Amesema Manjale Magambo.

Manjale ameongeza  ndani ya Chama hicho kumekuwepo na watu ambao wamekuwa wakikichafua chama cha Mapinduzi(CCM) na  kumchafua Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri za kimaendeleo ambazo amezifanya  na kwamba  wao kama vijana hawapo tayari kuona watu wanaendelea na uzalilishaji wa namna hiyo kwa viongozi na chama.

“Kuna wahuni baadhi wameingia kukivuruga chama chetu na sisi umoja wa vijana tumejitolea kucheza nao sahani moja ,hawa wahuni ambao wanajifanya wametumwa na Rais Samia tunawaambia waache mara moja kumchafua               Rais wetu na Geita nenda kamwambie kawaida tutakuwa na oparesheni hivi karibuni ya  kuwaondoa wahuni ndani ya Chama chetu,hatuwezi kuhishi na wahuni Samia ameshamaliza kila kitu mtu unakuja unasema unafanya tathimini ya uchaguzi chama kinautaratibu wake,hawa wahuni na wageni ndani ya chama hatutaki kuwasikia” Amesema Manjale Magambo.

Aidha Manjale amewataka vijana wenye uwezo wa kuongoza  kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali kwenye chaguzi ambazo zinakuja.

 




Share To:

JOEL MADUKA

Post A Comment: