Ferdinand Shayo ,Arusha .
Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation For Tomorrow (TFFT) limeendesha mashindano ya Mawazo bunifu ya kampuni zilizobuniwa na wanafunzi wa shule 11 za sekondari kutoka mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ambapo shule ya Arusha Science secondary imeibuka na ushindi na inatarajiwa kushiriki mashindano ya kimataifa yatakayofanyika nchini Maurtius Disemba Mwaka huu.
Mkurugenzi wa TFFT Noah Kayanda amesema mashindano ya uendeshaji kampuni na utekelezaji mawazo bunifu ya biashara yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto zinazoikabili jamii ikiwemo ajira na uharibifu wa mazingira.
“Tunatekeleza mashindano haya kwa kushirikiana na Junior Achievement Africa kupitia programu ya JA Company program ambayo inawasaidia vijana kupata elimu ya fedha ,usimamizi wa miradi ili kuwaandaa wanapohitimu shule kukabiliana na changamoto zilizoko kwenye jamii ikiwemo ajira” Anaeleza Mkurugenzi wa TTFT
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Emmanuela Kaganda amesema program hiyo itawasaidia kuwasaidia vijana katika Nyanja mbali mbali kuibua vipaji na ubunifu na kuongeza kuwa vijana wana ubunifu mkubwa unaoweza kuisaidia jamii na taifa kwa ujumla.
Kaganda amesema kuwa vijana wa kitanzania wana uwezo mkubwa na wanaweza kushinda katika Nyanja za kimataifa huku akiwataka wakuu wa shule kuendeleza ubunifu wa wanafunzi hao.
Wanafunzi wa Kikundi cha wanafunzi kilichofahamika kama Bloomtech kutoka shule ya Sekondari Arusha Science akiwemo Baraka Kileo na Naira Issa ambao wameibuka washindi wa mashindano wamesema wako tayari kuiwakilisha vyema Tanzania katika mashindano ya kimataifa yatakayofanyika Disemba mwaka huu nchini Mauritius.
Post A Comment: