Mkuu wa wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro Shaka Hamdu Shaka amepiga marufuku shughuli za uchimbaji holela wa madini, kilimo na ukataji miti hovyo kwenye chanzo cha maji katika Kata ya Malolo wilayani humo.
Shaka amesema hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji Malolo unaotekelezwa na Ruwasa , ambapo wananchi hao wamesema uchimbaji wa madini katika eneo hilo umekua kero na kusababisha uchafuzi wa maji .
Baada ya kupata malalamiko hayo Shaka amewataka wananchi kuacha tabia hiyo na atakaye kamatwa hatua za Kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Aidha Shaka amewataka wananchi hao kuwa walinzi wa miundombinu hiyo Ili iwanufaisha Kwa kipindi kirefu kizazi Cha Sasa na kijacho kwani serikali inatumia gharama kubwa kuwafikishia huduma hiyo wananchi
Anasema serikali imekua ikitekeleza ujenzi wa miradi Mbalimbali kwenye sekta ya maji hivyo baadhi ya watu wamekua na wakiharibu miundombinu hiyo.
"Dokta samia Suluhu Hasaan amekua akitoa fedha kwenye miradi ya maji hasa wilaya hii ya Kilosa hivyo lazima tutunze miundombinu hii na Kila mtu awe mlinzi wa mwezake" anasema
Awali mmoja wa wakazi wa Malolo Boazi Igombe ameishukuru Serikali Kwa ujenzi wa mradi huo kwani awali walikua wakipata huduma hiyo umbali mrefu Lakini Bado Changamoto ya shughuli za uchimbaji madini katika chanzo cha maji zinarudisha nyumba jitihada za serikali huku wakihofia Kupata magonjwa ya mlipuko.
Kwa Upande wake meneja Wakala wa maji safi na Usafi wa Mazingira (RUWASA) wilaya ya Kilosa Mhandisi Silvia Ndimbo amesema ujenzi wa mradi huo umegharimu kiasi cha Shilingi Bil.1 na utawanufaisha Wakazi zaidi elfu 13 wa vijiji vya Malolo A,Malolo B na Chabi.
Mradi wa maji Malolo umejengwa kwa kwa Fedha za COVID 19 na ulianza kutekelezwa mwaka wa fedha 2022/2023 chini ya mkandarasi Jeccs Contruction and Supplies limited na Sasa mradi imekamilika kwa asilia 100 tayari umeanza kutoa huduma kwa Wananchi.
Post A Comment: