Jukwaa la Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) likiongozwa na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Shabani Matwebe limeiomba Serikali ya Tanzania chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokubali kamwe kuingia kwenye mtego wa kufungia mtandao wa X (zamani Twitter).

Kauli ya Matwebe imekuja siku kadhaa baada ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) chini ya Mwenyekiti wake Mohammed Ali Kawaida kuitaka Serikali kupitia Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kufungia mtandao huo ikidai mtandao huo unaruhusu mambo ambayo ni kinyume na utamaduni wa Watanzania.

“Ni kama ilivyo Instagram, Facebook na YouTube, ‘X’ au Twitter ni sehemu ambayo Vijana wa Kitanzania wamekua wakilitumia Jukwaa hilo kujipatia riziki, JUMIKITA ipo tayari kushirikiana na Serikali kujua namna bora ya matumizi ya mitandao ya kijamii na inatoa ushauri Serikali isiingie kwenye mtego wa kufungia mtandao huo” ——— Shabani Matwebe.

Share To:

Post A Comment: