JOPO la Madaktari Bingwa na wabobezi wa magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya (Ocean Road) wameweka kambi Mkoani Arusha lengo ni kushiriki Kambi ya uchunguzi na matibabu inauoratibiwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda.


Akizungumza katika Kambi hiyo Meneja, Kitemgo cha Uchunguzi wa saratani na elimu kwa Umma wa Ocean Road Dk. Maguha Stephano amesema lengo la taasisi hiyo kushiriki Kambi hiyo ni kufikia azima ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kuboresho huduma za kitababu kwa wagonjwa wa Saratani.

Dk.Maguha alisema, kutoka na ukubwa wa tatizo la magonjwa ya saratani kwa sasa, watahakikisha wanatumi utaalamu waliona kutoa elimu bure na kuwafikia wananchi wengi katika kambi hiyo.

“Huduma hizi zimeamza Leo Juni 24 na itadumu hadi Juni 30, Ocean Road imeleta madaktari bingwa na wabobezi kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa na Rais wetu kusogeza huduma za uchunguzi na matibabu kwa wananchi,”alisema.

Alisema, wanaamini hatua hiyo itaenda kuokoa maisha ya watu wengi hususani wale ambao hawajawahi kufanyiwa uchunguzi.

“Kupitia kambi hii tutafanya uchunguzi wale watakaobainika kuwa na dalili za awali watafanyiwa uchunguzi zaidi na matibabu kwa haraka hivyo kuokoa maisha yao na wale ambao walikuwa hawazingatii matibabu watapewa ushauri ipo haja kubwa ya kila mmoja kufanyiwa uchunguzi na iwapo una tatizo kuzingatia matibabu,”alisema.

Alisema huduma zinazotolewa na taasisi hiyo katika kambi hiyo ni elimu, ushauri, huduma za kibingwa za uchunguzi na Matibabu ya saratani.

Dk. Maguha aliongeza kuwa, watakaogudulika kuwapo na saratani katika kambi hiyo pia, watapewa rufaa ya moja kwa moja kwenda Ocean Road Dar es Salaam, kwa ajili ya matibabu zaidi kwani Saratani ikigundulika mapema inatibika.



Share To:

Post A Comment: