Akizungumza na wazazi kuelekea siku ya mtoto wa Afrika Mkurugenzi wa kiserikali la Nachingwea Paralegal Aid Organization (NAPAO) ambaye ni msaidizi wa kisheria,Sabrina Dossa alisema kuwa wazazi lazima watambue haki za mtoto kama vile kumpa ulinzi,elimu na kumpa mahitaji yote muhimu kwa mtoto.
Wazazi wakipata elimu kutoka kwa afisa habari na mawasiliano wa kiserikali la Nachingwea Paralegal Aid Organization (NAPAO), Christopher Lilai akitoa elimu ya malezi kwa watoto
Afisa habari na mawasiliano wa kiserikali la Nachingwea Paralegal Aid Organization (NAPAO), Christopher Lilai akiongea na wazazi umuhimu wa malezi ya watoto.

Na Fredy Mgunda, Lindi.

KUTOKANA na kuongeza kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi shirika lisilo la kiserikali la Nachingwea Paralegal Aid Organization (NAPAO) imeamua kutoa elimu ya sheria ya mtoto kwa wananchi wa kijiji cha Mkonjela Chini ili jamii itambue haki za mtoto na wajibu wao katika malezi ya mtoto.


Akizungumza na wazazi kuelekea siku ya mtoto wa Afrika Mkurugenzi wa Shirika hilo lisilo la kiserekali ambaye ni msaidizi wa kisheria,Sabrina Dossa alisema kuwa wazazi lazima watambue haki za mtoto kama vile kumpa ulinzi,elimu na kumpa mahitaji yote muhimu kwa mtoto.


Dossa alisema kuwa wazazi wanapaswa kufichua matendo yote ya ukatili wa kijinsia,kama vile ulawiti, ubakaji na ndoa za utotoni ili kuwa na kizazi bora kwa faida ya familia na Taifa kwa ujumla.


Aliwataka wazazi ,walezi na jamii  kuwa makini katika malezi kwa kuwafunza watoto Mila na tamaduni zao na  kuwapatia mafundisho yenye maadili mema  kwa jamii na maisha yao kwa ujumla.


Kwa upande wake afisa habari na mawasiliano wa kiserikali la Nachingwea Paralegal Aid Organization (NAPAO), Christopher Lilai alieleza  kuwa shirika niatoa msaada kisheria,ushauri wa kisheria kwa jamii pamoja na usuluhishaji wa migogoro  kwa wananchi  ambao hawana  uwezo wa kifedha wa kugharamia.

"Shirika letu litoa huduma  za kisheria   bila malipo yeyote  kwa wale ambao hawana uwezo lengo ni  kumfanya mwananchi  apate haki yake bila kuathiriwa na umaskini"alisema Lilai.

Hivyo  alitoa wito  kwa kila mwananchi anaehitaji msaada huo  kufika katika ofisi zao au kwa wasaidizi wa kisheria waliopo kwenye kata 14.


Naye mmoja wa wazazi, wa kijijini hapo Zuhura Ungele ameeleza kuwa bahadhi ya wazazi wanawagopa watoto wao wanaosoma  sekondari hivyo kufanya watoto wengi huwadharau wazazi wao pindi wanapofikia elimu ya kidato cha nne (4) na kuendelea madai ya kujiona wao ni wasomi kuliko wazazi wao .

Hivyo kuelekea siku ya mtoto wa Afrika  aliwataka watoto  kujifunza na kuelewa thamani ya mzazi katika jamii 

Ungele alisema kuwa mwenendo wa maisha ya watoto wa siku hizi si mazuri kwani kwa asilimia kubwa yanakiuka maadili ya watanzania na kuwataka watoto wote kuanza kuwajibika kwa wazazi wao ili wapate malezi bora na mema kwa maisha yao.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: