Na Munir Shemweta, TABORA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amekitaka Chuo cha Ardhi Tabora (ARITA) kufanya maboresho kwenye sehemu yake ya uchapishaji ili kwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia.
Mhe Pinda ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki alipofanya ziara katika chuo hicho ikiwa ni jihudi zake za kuhakikisha chuo cha ARITA kinafanya kazi kwa ifanisi na kutoa huduma bora za uchapishaji.
Amesema, uboreshaji sehemu ya uchapishaji ndani ya chuo hicho kutakiwezesha chuo kupata kazi nyingi za uchapishaji na hivyo kukiingiza pesa.
" Hivi vifaa mlivyokuwa navyo ni vya kizamani sana na haviendani na teknolojia ya sasa labda kama vitaendelea kubaki kwa ajili ya kufundishia wanafunzi ili kujua tulikotoka lakini kwa kipindi hiki mnahitaji kuboresha ili muende sambamba na tekonolojia ya sasa" alisema Mhe. Pinda.
Naibu Waziri ameutaka uongozi wa chuo hicho cha Ardhi Tabora kuandika gharama za vifaa vya kisasa ili aoene namna ya kukisaidia kupata vifaa vya kisasa vitakavyokiwezesha chuo kuingia kwenye ushindani wa kibiashara.
Aidha, ameutaka uongozi wa chuo cha ARITA kwenda kuiifunza kwa taasisi nyingine kama vile Taasisi ya Uchapishaji ya Serikali (Government Printers) ili kuona namna bora ya kuimarisha sehemu hiyo ili kiweze kufanya vizuri kwenye utendaji kazi wake.
‘’Chuo hakina Afisa Miradi na lazima chuo kiwe na watu wanaohitajika kama wataalamu wa usimamizi wa miradi hivyo lazima ‘to change direction’ hii ni biashara. Lazima kuwa na mtazamo mpya kuhakikisha mamlaka ya chuo inatoa matokeo. Mnaweza kuona kama mnakwenda lakini mko katika mark time’’. Alisema Mhe. Pinda
Awali Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ardhi Tabora Juma Mkuki amemueleza Naibu Waziri Mhe. Pinda kuwa, chuo chake kinaendesha mafunzo pamoja na shughuli za uchapishaji kwa kushirikiana na wizara pamoja na wadau wegine ambapo chuo hicho kinazalisha machapisho mbalimbali kwa idara za serikali, taasisi na mashirika mbalimbali kama sehemu ya kujiongezea kipato.
Kwa mujibu wa Mkuki, kuanzia mwaka 2019/2020 hadi sasa chuo kinazlisha machapisho ya nyaraka mbalimbali zinazotumiwa na wizara ya ardhi kwa ajili ya kumilikisha ardhi na usajili kwa ujumla.
‘’Chuo kinatoa huduma kwa taasisi zingine ambazo zinatumia baadhi ya machapisho yetu ikiwa ni pamoja na vitabu mbalimbali na nyaraka zisizo za kiserikali’’. Alisema Mkuki.
Kaimu Mkuu huyo wa chuo cha Ardhi Tabora, amesema, sehemu ya uchapishaji inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maabara kwa ajili ya uchapishaji,
Hata hivyo, ameeleza kuwa, pamoja na chuo kujitahidi kutafuta mitambo na vifaa vya uchapishaji lakini jengo linalotumika ni dogo hivyo chuo hicho cha ARITA kiko kwenye hatua za kuhakikisha jengo hilo linajengwa kwa kushirkiana na wadau nje ya chuo.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akikagua moja ya mashine ya uchapishaji ya muda mrefu kwenye chuo cha Ardhi Tabora wakati wa ziara yake katika chuo hicho mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ardhi Tabora Juma Mkuki.
Mtaalamu katika chumba cha uchapishaji kwenye Chuo cha Ardhi Tabora (ARITA) akifafanua jambo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda mwishoni mwa wiki.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akipata maelezo kuhusiana na mashine ya muda mrefu katika chuo cha Ardhi Tabora wakati wa ziara yake kwenye chuo hicho mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ardhi Tabora Juma Mkuki.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akiwa katika chumba cha uchapishaji wakati wa ziara yake kwenye Chuo Ardhi Tabora mwishoni mwa wiki.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akiwa katika chumba cha uchapishaji wakati wa ziara yake kwenye Chuo Ardhi Tabora mwishoni mwa wiki.
Post A Comment: