Serikali ya Tanzania imeuhakikishia Umoja wa Posta Afrika (PAPU) kuhusu msimamo wake usioyumba wa kuendelea kuunga mkono na kusaidia mipango mkakati ya Umoja huo, kwa maendeleo ya Sekta ya Posta Afrika.

Hayo yamesemwa leo mkoani Arusha na  Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi  wakati akifungua mkutano wa 42 wa Baraza la Utawala la PAPU, unaofanyika Makao Makuu ya Umoja huo jijini Arusha.

“Kwa heshima kubwa, napenda kuthibitisha msimamo usioyumba wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kusaidia mipango mbalimbali ya PAPU,” amesema Mhandisi Mahundi.

Mhandisi Mahundi ameutaka mkutano huo wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika (PAPU), kutafakari njia mbalimbali zitakazowezesha mageuzi ya posta Afrika, ili kuendana na maendeleo ya kasi ya biashara mtandao (e-commerce) pamoja na mabadiliko makubwa ya teknolojia ya mawasiliano na dijitali.

Ameongeza kuwa ,katika Afrika, Posta inafanya kazi kubwa ya kutoa huduma ya kuaminika na uhakika, na huduma yenye tija kwa biashara kubwa, ndogo na za kati (MSMEs) na ni vizuri kwamba wakati dirisha la biashara mtandao likiwa limefunguka na kuja na fursa zaidi, tayari baadhi ya Posta Afrika zimeanza kujishughulisha na kutoa huduma mbalimbali katika mnyororo wa biashara mtandao.






Share To:

Post A Comment: