Na Joel Maduka,Geita..
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
CCM ,Mkoa wa Geita,Nicholaus Kasendamila amefunga rasimi mafunzo ya itikadi kwa
vijana wa CCM ,huku akisisitiza suala
zima la vijana kuzingatia usalama wao
wenyewe na usalama wa Nchi.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita
ametoa Wito huo wakati akizungumza na zaidi ya vijana mia sita ambao walikuwa
kwenye mafunzo ya itikadi ambayo yamefanyika Kata ya Nyakagomba Wilayani Geita.
Amesema wao kama vijana
wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kujilinda na vitendo viovu ambavyo vinaweza
kuhatarisha maisha yao ya sasa na baadae.
“Natambua vijana nyie bado Taifa
linawaitaji na bado mnanguvu Kubwa kwa Taifa letu lakini niwaombe sana
zingatieni suala la usalama wenu na wa Nchi vijana wengi wamepotea sababu ni
kukosa nidhamu na kujikuta wakijiingiza kwenye makundi ambayo yameendelea
kugharimu maisha yao ya kila siku”Amesema Nicolaus Kasendamila.
Naye Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Geita Manjale Magambo amesema uwepo wa makambi ya vijana yamekuwa na faida nyingi kwa vijana kutokana na kuwajengea uwezo wa kujitegemea na kujikwamua kiuchumi na kusaidia kukijua chama zaidi kutokana na mafunzo ya Historia ambayo yanatolewa.
Post A Comment: