Na  Elinipa Lupembe

Halmashauri ya Monduli imeendelea kufanya vizuri katika kutakeleza majukumu yake kwa  kuzingatia kanuni, sheria na taratibu za mapato na matumizi ya fedha za Umma pamoja na usimamizi wa miradi ya maendeleo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Mhe. Isack Joseph, wakati akifungua Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani la kupitia taarifa za Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za halmashuri hiyo, mwaka wa fedha 2022\/2023, uliofanyia Juni 14, 2024.

Mhe. Joseph amesema kuwa, kwa ushirikiano uliopo baina ya Madiwani na Watalamu wa ngazi zote wameendelea kutekeleza majukumu yao na kuhakikisha Hoja zote za ukaguzi, zinafanyiwa kazi kwa kuzingatia vigezo na hadi kufikia Hoja 8 kutoka hoja kati ya 160 mpaka 180 kwa miaka ya nyuma.

Ameweka wazi kuwa, Hoja zote zimepitiwa na wajumbe kwa kushirikiana nawatalamu kwenye vikao vya kisheria na kwa mwaka huu, asilimia kubwa Hoja zimefungwa tofauti na miaka ya nyuma ambapo halmashauri ilikuwa na hoja kati ya 160 mpaka 180 hoja ambazo hazijafungwa.


Mhe. Joseph amefafanua kuwa ni hali ya kujivunia sana kwa madiwani na watalam wa halmashauri hiyo kwa ushauri wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha pamoja na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Kanda kwa kufanya kazi kubwa ya kujibu Hoja kwa aslimia kubwa na hatimaye zimesalia hoja 17.


"Miaka ya nyuma tulikuwa na Hoja zaidi ya 160 mpaka 180, tulikuwa kwenye hali mbaya sana lakini kwa mwaka 2022\/2023 halmashauri yetu ina Hoja nane tu ambazo ziko kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji, tunategemea mwaka ujao wa fedha kufikia  sifuri"


Aidha, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita, kwa kazi kubwa anayoifanya kwenye wilaya ya Monduli kwa kutoa fedha nyingi zilizotekeleza shughuli na miradi ya maendeleo katika sekta za maji, barabara, afya, elimu pamoja na utawala, miradi ambayo imerahisisha upatikanaji na utoaji wa huduma kwa wananchi wa Monduli.

Zaidi ameishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa usimamizi mzuri wa kazi ambayo imewezesha ujenzi wa jengo jipya la utawala halmashauri ya Monduli, jengo ambalo limewarahisishia wananchi kupata huduma.



















Share To:

Post A Comment: