Na Joel Maduka ,Geita
Mjumbe wa Halmashuri
kuu ya CCM Taifa , MNEC Chacha Wambula
(WAJA) akiwa wilayani Bukombe Mkoani Geita amewataka vijana kutojiingiza katika
Makundi yasiyofaa kwani yanaweza kuleta athari Kubwa kwenye Jamii.
Hayo ameyasema wakati
alipokuwa akifunga Makambi ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)
wilaya ya Bukombe yaliyodumu kwa kipindi cha siku sita Wilayani humo
huku akiwataka vijana hao kuzingatia yale yote waliyofundishwa yaweze
kuwa na tija kwa Jamii na pamoja na chama cha Mapinduzi(CCM).
Aidha Mnec Chacha
amewataka vijana kuzingatia suala zima la uzalendo kwa Nchi na kutangaza
matendo mema ambayo yamefanywa na Serikali ya awamu ya sita(6),huku akisisitiza
uwajibikaji na uchapakazi kwa vijana.
“Niwaombe vijana wangu
najua hapa mmefundishwa mambo mbalimbali yakiwemo ya ujasiriamali nendeni
mkatumie yale ambayo mmefundishwa kwenda kuanzisha miradi ya kiuchumi mimi nipo
tayari kuwasapoti wale ambao wataitaji msaada wangu”Amesema Chacha Wambura.
“Mimi nimaamini katika
vitu vitatu uchapakazi,kuwa mwaminifu na kuwa muwazi kama unavitu hivi leo hii
uwezi kukosa kazi lakini kama wewe kitu kimoja wapo kinakosekana hata ukifanya
kazi utaondolewa kazini,Elimu ni kitu kingine unaweza kuwa na elimu na ukakosa
hivi vitu elimu yako isikusaidie”amesema Chacha Wambura.
Aidha
Mnec Chacha amewaomba vijana kujifunza desturi ya utii kwani sio utumwa kwa kijana kuwa mtii na
kuheshimu mamlaka muhimu ambazo zimewekwa na Nchi pamoja na serikali.
Post A Comment: