Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Fatma Toufiq ametoa mitungi ya gesi 200 kwa wanawake wajasiriamali wa wilaya ya kongwa 

Toufiq ametoa mitungi wajasiriamali hao akiwa na lengo la kuendelea kuiunga mkono serikali katika jitihada za kuhamasisha wananchi kutumia nishati safi pamoja na kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa ambao umekuwa ukisababisha madhara kwa watumiaji.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi mitungi hiyo Mbunge toufiq amesema anatamani kuona wanawake wajasiriamali wanakuwa chachu ya utunzaji wa mazingira kwa kuingia kwenye matumizi ya gesi kuliko kuendelea kuharibu mazingira kwa kutumia kuni pamoja na mkaa.

Amesisitiza kuwa, Rais Samia ameanzisha kampeni ya nishati safi yenye lengo la kumtua mzigo wa kuni mwanamke na hatimaye kumpa muda mwingi katika kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo hasa kwa kutambua mwanamke ndiyo nguzo ya familia.







Share To:

Post A Comment: