Na Dickson Mnzava, Same.

Maono ya Jumuiya ya wazee wilayani Same Mkoani Kilimanjaro ya kuanzisha Bank ya wananchi imeanza kuzaa matunda baada ya kamati anzilishi kuanza kuratibu shughuli mbalimbali za uanzilishi wa bank hiyo ya wananchi ambayo inatajwa kugusa maendeleo ya jamii ya Same na kuongeza kipato kwa kaya.


Maono hayo ya kuanzisha Bank ya wananchi yaliibuliwa mwaka jana November wakati wa mkutano Mkuu wa Jumuiya ya wazee wilayani Same ambapo wazee hao walienda mbali zaidi na kuona maono hayo ili kuweza kuleta maendeleo na fursa za kiuchumi kwa wananchi wao.


Wakizungumza kwenye kikao kazi cha kuratibu shughuli mbalimbali za uanzilishi wa bank hiyo mratibu wa kamati hiyo Samweli Nyiru amesema maono yao nikutaka kuwaletea wananchi wa Same maendeleo hivyo wanaamini ndoto hizo zitakuwa na matokeo chanya kwa jamii ya Same katika kukuza pato lao.


Nyiru amesema uwepo wa bank ya wananchi itachochea ukuaji wa maendeleo wilayani Same pamoja na kuleta usalama wa pesa za wananchi kwani bank hiyo itakuwa niya wananchi hivyo wataweza kuwa na uwanda mpana katika kuwekeza hisa zao na kufanya shughuli mbalimbali za uchumi.

"Haya ni maono ya Jumuiya ya wazee wilayani Same JUWASA baada ya kukutana kwenye mkutano Mkuu wa Jumuiya mwaka jana November swala hili liliibuliwa na wazee na likapokelewa kwa namna yake ambapo wazee waliona hakuna kuliweka chini tena bali hatua zianze kuchukuliwa na wakateuliwa wajumbe wa kuratibu shughuli hii na wamekaa na kuchagua kamati anzilishi ambayo sasa ipo kazini kuaanda katiba na hatua zingine kuanza".

"Alisema Samweli Nyiru".


Naye mwenyekiti wa kamati hiyo Rehema Mshana amesema watakimbizana na muda kuhakikisha bank hiyo inaanza haraka iwezekanavyo na itakuwa bank ya wananchi wote wa Wilaya ya Same na itakuwa mkombozi kwa wananchi ambao wamekuwa wakipatiwa mikopo kwenye taasisi ambazo zimekuwa kikwazo kikubwa kwenye familia nyingi kama vile mikopo ya kausha damu.


Mwisho.

Share To:

ASHRACK

Post A Comment: