Dkt Stanford Mwakatage kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Lindi Manispaa akizungumzia utekelezaji bora mpango wa wahudumu wa afya ngazi ya jamii ndani ya Manisapaa ya Lindi, watendaji wa kata 31, watendaji wa Mitaa 117 , watendaji wa Vijiji 47 waganga wafawidhi 52 pamoja na vitongoji 236 wapata mafunzo ya utekelezaji na miongozo .

Na Fredy Mgunda, Lindi.

Katika kuhakikisha utekelezaji bora mpango wa wahudumu wa afya ngazi ya jamii ndani ya Manisapaa ya Lindi, watendaji wa kata 31, watendaji wa Mitaa 117 , watendaji wa Vijiji 47 waganga wafawidhi 52 pamoja na vitongoji 236 wapata mafunzo ya utekelezaji na miongozo .


Akifungua Mafunzo hayo Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi ambaye pia ni mganga mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Dkt. Stanford Mwakatage  amesisitiza uadilifu katika kufanya uchaguzi wa watoaji huduma ngazi ya jamii CHWs ili tuweze kupata watoa huduma wenye weledi  katika kuboresha huduma ili kufikia azma ya Afya kwa wote kufikia mwaka 2030.


Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Afisa kutoka wizara ya Afya ngazi ya jamii  Bi Orsolina Tolage 

amesema mafunzo hayo yanakwenda kuleta tija kwa jamii hivyo kila mmoja azingatie utaratibu na miongozo inayotolewa.


Mkoa wa Lindi, unatarajiwa kupata watoa huduma zaidi ya 4,000 kutoka halmashauri ya Lindi Manispaa, Nachingwea, Liwale, kilwa, Mtama na  Ruangwa .


Akizungumza mara baada ya Mafunzo hayo Zuwena Hamis Mtendaji wa mtaa amesema mafunzo hayo yamewapa mwanga wa kile ambacho kinapaswa kufanyika


"Nashukuru kwa mafunzo haya kwani sasa yametujengea uwezo na kutupatia mwanga wa kufanya kazi kwa weledi mkubwa " Bi Zuwena Hamis Mtendaji


Ikumbukwe kuwa mkoa wa Lindi ni miongoni mwamikoa 10 ya mwanzo katika utekelezaji wa mpango huu ambapo Halmashauri ya Lindi Manispaa na Mtama zimeanza utekelezaji kwa wadau wake kupata mafunzo na utekelezaji.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: