"Timu ya madaktari wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido tumejiandaa na tumejipanga vema kusaidia na kutoa huduma bora kwa wananchi wote wa Wilaya ya Longido zikiwepo huduma za upasuaji".Alisema Daktari D Majani Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Longido.

Halmashauri ya Wilaya ya Longido kupitia idara ya afya, Ustawi wa Jamii na Lishe katika kuboresha huduma ya mama na mtoto pamoja na kusogeza huduma karibu na wananchi.

Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake Rais Dkt Samia Suluhu imejenga vituo vya Afya vingi kote nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma mahala pa karibu pasipo kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo muhimu za Afya

Sambamba na kutoa vifaa tiba kwa ajili ya kutolea huduma hizo kwa wananchi.

Kwa kuona na kuzingatia hilo kituo cha Afya cha Engarenaibor kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Longido kimeanza kutoa huduma za upasuaji kwenye kituo hicho kwa mara ya kwanza.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi na mkazi wa Engarenaibor mama Nanyori Amempongeza Mheshimiwa Rais kwa kuwajengea kituo hicho na kuwapatia Madaktari sambamba na vifaa tiba.

"Sisi wananchi na wakazi wa Engarenaibor tunapenda kutoa shukrani zetu zifike moja kwa moja kwa Mama yetu mama Samia kwa kutupigania sisi wakazi wa Engarenaibor kwa kujenga Kituo cha Afya kizuri." Alisema mama Nanyori

"Tunapenda kuipondeza serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Dr Samia kwa kuwezesha miundombinu mbinu na vifaa tiba  hatimae huduma ya upasuaji imefanyika katika kituo cha afya Engarenaibor kwa mara ya kwanza tarehe 13/06/2024 hii inapelekea kuwapunguzia akina mama usumbufu wa kusafiri takrbani km 40 kwenda hospital ya wilaya pindi wanapokubwa na changamoto za uzazi". Alisema Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt D Mathew Majani.

Kituo cha Afya Cha Engarenaibor kinatoa huduma zote muhimu za kiafya, pamoja na hata huduma ya mama na mtoto.

Aidha wananchi na wakazi wote wa Engarenaibor na Longido kwa ujumla ni rai ya Serikali kutaka wananchi wote wanaenda kupata huduma ya Afya kwenye vituo vilivyowekwa na Serikali na kuacha kabisa tabia ya kutumia miti shamba na kujifungulia njiani,kwani inahatarisha sana maisha ya wananchi walio wengi hasa wazee, wamama wajawazito pamoja na watoto.

Huduma za Afya kwenye Hospital, vituo vya Afya na Zahanati zilizopo Wilayani Longido ni bora  na zina madaktari wazuri na wenye weredi wa kutoa huduma hizo.

Share To:

Post A Comment: