Katika kipindi cha hivi karibuni, sekta ya sukari nchini imekuwa ikikumbwa na changamoto nyingi, hususan suala la bei za sukari kupanda kiholela. Viwanda vya sukari viliongeza bei ya sukari na kukataa kushusha licha ya kupata msaada wote kutoka kwa serikali. Hali hii ilifikia kilele wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, ambapo bei ya sukari ilipanda kutoka TZS 2,500 kwa kilo moja hadi TZS 4,000 na hadi 6000 maeneo mengine kwa kilo moja, na kusababisha malalamiko mengi kutoka kwa wananchi.

Serikali iliamua kuchukua hatua kali ili kudhibiti hali hii kwa kutoa vibali vya uagizaji wa sukari kwa wafanyabiashara wengine sokoni. Hatua hii ilileta matokeo chanya kwani bei za sukari zilianza kushuka kutoka TZS 4,000 kwa kilo moja hadi TZS 2,800 kwa kilo moja. Hata hivyo, serikali iliona haja ya kuchukua hatua zaidi kwa kuandaa sheria bungeni za kuvunja ukiritimba wa viwanda vya sukari. 

Kwa manufaa ya wamiliki matajiri watano wa viwanda vya sukari, serikali haiwezi kushikilia mateka watu wake milioni 65.

Kwa lengo la kushinikiza serikali kubatilisha mabadiliko hayo, wamiliki wa viwanda hivyo walirejea katika vitendo vyao vya kifisadi kwa kuhonga wabunge wala rushwa kama Mpina ili wapige kelele dhidi ya hatua hizi.

Ni nini kibaya ikiwa kampuni ndogo au kubwa ziliruhusiwa kuagiza na kuuza sukari sokoni ili kushusha bei? 

Je, ni kampuni kubwa kama Metl na Super Doll pekee ndizo zinazostahili fursa ya kuagiza na kuuza sukari? 


Mpina anazungumza upuuzi gani? 


Huu ni ulimwengu wa wazi wa mitandao ya kijamii na watu ni werevu na wanaelewa kila kitu.

Viongozi wakuu wa CCM wanapaswa kuhakikisha kuwa Mpina anaomba radhi na anajiuzulu kwa kuunga mkono waziwazi hujuma dhidi ya nchi na watu wake. 

Swali la kujiuliza, Je, mnataka serikali isichukue hatua yoyote huku makundi ya kifisadi yakiendelea kuwanyonya wananchi wake? 

Ni dhahiri kuwa tatizo hili lingeachwa bila kudhibitiwa, gharama kwa uchumi ingekuwa kubwa sana. 

Mfumuko wa bei ya sukari ungeathiri sekta mbalimbali za uchumi, kuongeza gharama za maisha kwa wananchi na kupunguza uwezo wa kununua bidhaa nyingine muhimu. Hii ingeweza kusababisha madhara makubwa kwa ustawi wa kiuchumi wa taifa.

Ni wakati wa kusema hapana kwa hujuma na kulinda maslahi ya wananchi. Serikali ipo kwa ajili ya wananchi na itahakikisha haki inatendeka kwa wote.

Share To:

Post A Comment: