Ashrack Miraji Same Kilimanjaro
Same, Kilimanjaro, Tanzania
Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni, ametoa pongezi kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dk Emmanuel Nchimbi, kwa kutoa wito kwa Watanzania kuhifadhi tunu ya umoja wa kitaifa na amani ya Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mgeni alisisitiza umuhimu wa kuendelea kulinda amani wakati tunapoelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mgeni aliongeza kuwa siasa inapaswa kuwa chombo cha kuleta maendeleo ya Taifa na kuwahimiza wanachama wa vyama vya siasa kushikamana kwa pamoja.
Alisisitiza kuwa rushwa inaharibu jamii na kuwataka wananchi kuwa wazalendo katika kazi zao na kutoa wito kwa kiongozi yeyote asijihusishe na vitendo vya rushwa.
Kwa dhati, Mgeni aliahidi kufanya kazi kikamilifu kudhibiti mianya ya rushwa, hasa wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa.
Post A Comment: