Na Elinipa Lupembe

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Emmanuela Kaganda ameupongza uongozi wa Halmashauri ya Meru, watalamu na Madiwani kwa kufanyakazi kwa ushirikiano, ambao matunda yake yanaonekana kwa halmashauri hiyo kwa kupata Hati Safi kwa miaka 3 mfululizo.

Mhe. Emmanuella ametoa pongezi hizo wakati akizungumza kwenye Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani wa kujadili Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2022\/2023, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo leo Juni 14, 2024.

Ameweka wazi kuwa, halmashauri ya Meru imeendela kufanya vizuri katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na usimamizi wa fedha za serikali unaozingatia viwango, na kuwezesha kupungua kwa kiasi kikubwa cha Hoja za ukaguzi ukilinganisha kwa miaka ya nyuma.

"Niwapongeze watalamu, waheshimiwa madiwani, viongozi wa Chama,  wananchi wote wa Meru kwa umoja wenu kwa kuhakikisha, miradi inatekelezwa kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa huku wananchi wakifurahia matunda ya serikali yao ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani yenye malengo ya kusogeza huduma zote za kijamii kwenye maeneo yao" Amebainisha Mkuu huyo wa wilaya 

Amewasisitiza watalamu na viongozi kuendelea kushirikiana ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kwa kutekeleza ilani ya CCM yenye lengo la kufikisha huduma za jamii kwa wananchi, huduma zitakazotatua kero zao.

Hata hivyo, Mhe.Emmanuela ameahidi kufuatilia kesi ya deni la fedha la shilingi milioni 32.4 ya mwaka 2018 kati ya Halmashauri ya Meru na watumishi wawili, kesi ambayo halmashauri imeshindwa, jambo ambalo Waheshimiwa madiwani hawakuridhishwa na kushindwa kwa kesi hiyo ambayo waliamini ilikuwa na viambatanisho vyote vya kushinda.

"Nikukuombe Mhe. Mwenyekiti na Baraza lako, kubeba dhamana ya kurudi kufuatilia upya kesi hiyo, kwa kuwakuatanisha TAKUKURU na watalamu wa sheria ili kuona namna ya kukata rufaa kwa kesi hiyo na fedha hizo za wananchi ziweze kurudishwa na kufanya shughuli nyingine za maendeleo" Amesisistiza Mhe. Emmanuela

Awali kesi hiyo ni miongoni mwa hoja ya ukaguzi ambayo haikuwa imejibiwa.









Share To:

Post A Comment: