Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Comrade Daud Yassin akihutubia wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Iringa, viongozi pamoja wapiga kura kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Comrade Daud Yassin akijadilia jambo na viongozi wa CCM wilaya ya Kilolo.


Na Fredy Mgunda, Iringa.

MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Iringa Comrade Daud Yassin kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM wanatakiwa kuwa wamoja ili waweze kushinda kwa kishindo.


Yassin alisema kuwa kila kiongozi wa CCM mkoa wa Iringa anatakiwa kutimiza wajibu wao ili kuendelea kuimalisha umoja na mshikamano walionao sasa hadi uchaguzi iishe kwa ushindi mkubwa wa kishindo 



"Serikali ya CCM inayo ongozwa na Dk Samia Suluhu Hassan* ni Serikali ya wananchi. Kazi yetu ni kuhakikisha changamoto na kero za wananchi tunazitafutia ufumbuzi," amesema Yassin.



Aidha amewaambia Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Kata ya Nyalumbu kuhakikisha kuwa wanawachagua  wagombea wenye sifa na wanaokubalika kwa wananchi na amekemea mtindo wa kuweka maslahi binafsi badala ya maslahi ya chama. 


"Ikitokea mtu anakubalika na wananchi, tuweke pembeni tofauti zetu na tukipiganie Chama Cha Mapinduzi, chama kwanza sisi baadae,"

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: