Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt.Mwigulu Nchemba (Mb) ameongoza Mkutano wa 16 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi (SCFEA) na mkutano wa Mashauriano ya Kibajeti wa Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mhe. Dkt. Chemba amefungua kikao hicho kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango wa Sudani Kusini, Mhe. Mhandisi Awow Daniel Chuang Deng, ambaye ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Baraza hilo.
Baraza hilo limefanyika leo tarehe 17 Mei 2024, jijini Arusha, nchini Tanzania, ambapo Mawaziri hao wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo Wasilisho la nchi Wanachama kuhusu Miongozo ya Bajeti kwa mwaka wa Fedha 2024/2025 na Kaulimbiu za bajeti kwa mwaka wa Fedha 2024/2025.
Viongozi wengine walioshiriki Mkutano huo kwa upande wa Tanzania, ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato (Mb), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Alphayo Kidata, Maafisa na wataalam wengine kutoka Serikalini.
Post A Comment: