Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na Rais wa Kampuni ya Utalii ya Yingke (Yingke Group), Mei Xiang Rong kuhusu kushirikiana katika Sekta ya Utalii hasa utangazaji utalii, utalii wa mikutano pamoja na kuwekeza nchini Tanzania katika Sekta hiyo kwenye kikao kilichofanyika Ubalozi wa Tanzania nchini China leo Mei 14,2024.


Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu,Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, wajumbe wa Kamati ya Rais ya Kuitangaza Tanzania akiwemo Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Fatma Mbarouk, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Anderson Mutatembwa pamoja na watendaji na wawakilishi kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Wakala ya Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA).


Waziri Kairuki yuko nchini China kwa ajili ya kushiriki katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Kidiplomasia kati ya Tanzania na  China pamoja na uzinduzi wa mwaka wa Utalii na Utamaduni na pia uzinduzi rasmi wa filamu ya “Amazing Tanzania” utakaofanyika Mei 15, 2024.






Share To:

Post A Comment: