Wazee wa Kimila wa Kata ya Chela Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama ,Mkoani Shinyanga ,wamemsimika Mbunge wa Jimbo la Msalala ,Mhe Iddi Kassim Iddi kuwa Mtemi wa utemi wa Chela ambao unakusanya Vijiji 9.Ambapo wamempatia  Jina la Nkumbi.

Hatua ya wazee hao wa Kimila kumpa utemi Mbunge Iddi inatokana na Jitihada ambazo ameendelea kuzifanya katika kuwatumikia Wananchi Pamoja na kutatua Changamoto Mbalimbali ambazo zinawakabili Wananchi kwenye maeneo mbalimbali Ndani ya Jimbo la Msalala.


Share To:

JOEL MADUKA

Post A Comment: