Viongozi wa masoko ya biashara ya Jijini Dodoma wamepata mafunzo ya siku tatu ya kujengewa uwezo juu ya usimamizi wa uendeshaji masoko na usimamizi wa biashara yaliyoandaliwa na Jiji la Dodoma kwa ushirikiano na Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo.
Akifungua mafunzo hayo Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde amewataka viongozi hao kutumia elimu watakayopata kuongoza na kusimamia masoko Jijini Dodoma kwa uweledi mkubwa ili kusaidia kuboresha huduma kwa wateja na kuwaratibu vizuri wafanyabiashara hao.
Aidha Mbunge Mavunde alisisitiza juu ya usafi na utunzaji wa mazingira katika maeneo ya biashara na kuahidi kuwapatia viongozi hao wote vitendea kazi vya computer na photocopier katika ofisi zao ili kuboresha utoaji wa huduma.
Akizungumza katika Mafunzo hayo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini Cde Charles Mamba amelipongeza Jiji la Dodoma kwa kuandaa mafunzo hayo kwa viongozi wa masoko na kutaka kufanyika kwa mafunzo ya aina hii mara kwa mara ili kuwajengea uwezo viongozi.
Naye Mkuu wa Wilaya wa Dodoma Jabir M. Shekimwei amesema kwamba serikali inaendelea na zoezi ukarabati wa miundombinu na ujenzi wa masoko mapya kwa lengo la kusogeza huduma kwa Wanadodoma na kuchukua fursa hiyo kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mradi mkubwa wa TACTIC ambao umelenga kuboeresho miundombinu ya barabara na masoko Jijini Dodoma.
Post A Comment: