Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema Serikali imekusudia kuanzisha huduma mpya za upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu kwa kutumia akili mnembo (ROBOT) katika Taasisi ya Taifa ya Mifupa MOI

Akizungumza wakati wa uwasilishaji wa Bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2024/25 Bungeni jijini Dodoma leo, Jumatatu Mei 13, 2024 ambapo amesema serikali inakwenda kuandika historia hiyo (ya kufanya upasuaji kwa kutumia Robotic surgery) katika Taasisi ya Taifa ya mifupa (MOI)

Sambamba na hilo Waziri Ummy amesema Hospitali ya Kanda Bugando pia inakwenda kuanzisha huduma za upandikizaji wa figo, wakati Hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Benjamin Mkapa ziko mbioni kuanzisha huduma ya upandikizaji wa ujauzito 

Waziri Ummy amesema wanawake wengi wamekuwa wakitamani kupata mtoto/watoto lakini wanashindwa kumudu gharama kutokana na kwamba baadhi ya Hospitali binafsi zinazotoa huduma hizo zimekuwa zikiweka kiwango cha juu cha gharama, hivyo hatua ya huduma hizo kutolewa kwenye Hospitali za umma itapelekea wanawake wanye matamanio hayo kupata huduma hizo kwa gharama nafuu 

Aidha, katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Serikali kupitia Wizara ya Afya inakusudia kununua mtambo wa Cathlab utakaofanikisha kufanyika kwa upasuaji wa moyo bila kufungua kifua, huduma kama hiyo pia itapatikana kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amesema Taasisi ya Saratani ya Ocean road inakwenda kuanzisha kituo cha Saratani Mbeya, wakati Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete iko mbioni kufungua tawi la huduma hiyo kwenye Hospitali ya Kanda Chato kwa ajili ya wakazi wa maeneo ya Kanda ya Ziwa na viunga vyake

Serikali kupitia Wizara ya Afya imeahidi kuendelea kutoa huduma za ubingwa na ubingwa bobezi kwenye Hospitali mbalimbali za umma nchini sambamba na uboreshaji wa miundombinu ya maeneo ya kutolea huduma za afya nchini



















Share To:

Post A Comment: