Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda amekemea tabia ya malumbano na kuvutana kwa watumishi na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha suala ambalo limekuwa likisababisha kukwama kwa miradi mingi ya maendeleo licha ya Serikali kutoa fedha nyingi za kutekeleza miradi hiyo.

Mkuu wa Mkoa ametoa kauli hiyo ofisini kwa Mkuu wa Wilaya mara baada ya kupokea ripoti ya utendaji wa Wilaya ya Arusha, ripoti iliyoonesha kukwama kwa miradi mingi ya maendeleo kutokana na mabishano, malumbano na kutokuelewana kati ya Menejimenti ya Wilaya, Baraza la madiwani na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini.

Felician Mtahengerwa, Mkuu wa Wilaya ya Arusha amemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa migongano hiyo ja kutokuelewana kati ya viongozi wa kuteuliwa na kuchaguliwa kumesababisha adhabu kubwa kwa wananchi kutokana na miradi muhimu kukwama na hivyo kuwachelewesha kimaendeleo.

Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Christian Makonda amewaambia viongozi hao kuwa ingekuwa ni mamlaka yake angeivunja Mamlaka hiyo ya Jiji akihoji umuhimu wa Jiji kuwepo katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Jiji la Arusha.

Kufuatia hali hiyo Mhe. Mkuu wa Mkoa amelitaka pia Baraza la Madiwani Jiji la Arusha kujitafakari na kuamua kuwa sauti ya wananchi kikamilifu na kupambana kuhakikisha maendeleo ya watu yanapatikana kwa kukamilisha miradi yote ya maendeleo kwa wakati.












Share To:

Post A Comment: