Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2024 Godfrey Mnzava ameweka jiwe la msingi katika barabara ya kiwango cha lami ya smart lodge na angaza iliyogharimu kiasi cha shilingi millioni 

598,883,775.00. akiwa sambamba na mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo 

Meneja wa TARURA wilaya ya Nachingwea Mhandisi Enock Mshiha akisoma taarifa kwa viongozi wa mwenge wa uhuru kitaifa 2024
Viongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa na viongozi wa wilaya ya Nachingwea wakiongozwa na mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo wakikagua barabara ya kiwango kwa lami
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akikabidhiwa mwenge wa uhuru kitaifa kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Liwale.


Na Fredy Mgunda, Nachingwea.

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2024 Godfrey Mnzava ameweka jiwe la msingi katika barabara ya kiwango cha lami ya smart lodge na angaza iliyogharimu kiasi cha shilingi millioni 
598,883,775.00.

Akizungumza wakati wa kutoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa barabara hiyo Mhandisi Enock Mshiha alisema  mradi wa ujenzi wa  barabara za Smart lodge (0.51km) na Angaza (0.19km) kwa kiwango cha lami uliotekelezwa na Mkandarasi  Wanyumbani Construction Co. Ltd na gharama ya Tshs. 598,883,775.00 baada ya mapitio na kupunguza baadhi ya kazi ili kukidhi ukomo wa bajeti. 

Mhandisi Mshiha alisema kuwa Mradi huu kwa awamu hii ya kwanza, ulipangwa kutekelezwa kwa muda wa miezi sita (06) kuanzia tarehe 14/09/2023 na ulipaswa kukamilika kabla au ilipofika tarehe 13/03/2024, lakini kutokana mvua nyingi za msimu wa mwaka 2023/2024 zilizoanza kunyesha mwezi Disemba, 2023 mradi ulishindwa kukamilika ndani ya muda uliopangwa awali, hivyo Mkandarasi aliomba kuongezwa muda ambapo aliongezwa muda wa nyongeza wa siku sitini (60) kuanzia tarehe 14/03/2024 hadi tarehe 13/05/2024.

 hata hivyo mradi ulikamilika rasmi tarehe 12/04/2024 na kwa sasa mradi upo katika kipindi cha matazamio (Defects Liability Period) cha mwaka mmoja hadi tarehe 11/04/2025.


Alisema kuwa faida za mradi huo ni kuboresha mandhari ya mji wa Nachingwea na kupunguza gharama za matengenezo ya mara kwa mara.Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, 2024.

Mhandisi Mshiha alisema kuwa Wananchi wa Wilaya ya Nachingwea wanatoa shukrani za dhati kwa Serikali yao inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha za miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabaraNdugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, 2024 sasa tunakuomba utuwekee jiwe la msingi katika mradi wetu huu.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: