Na Ashrack Miraji Msumba News

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe pamoja na Viongozi wa Taasisi ya Care International wakati alipowasili Hyatt Regency Jijini Dar es salaam kufungua Mkutano wa Kimataifa wa Viongozi wa Taasisi hiyo tarehe 13 Mei 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati akifungua Mkutano wa Viongozi wa Kimataifa wa Taasisi ya Care International uliofanyika Hyatt Regency Jijini Dar es salaam tarehe 13 Mei 2024.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe , Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhandisi Amani Mafuru katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Taasisi ya Care Internation mara baada ya kufungua Mkutano wa Taasisi hiyo uliyofanyika Hyatt Regency Jijini Dar es salaam tarehe 13 Mei 2024

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Care International Marekani Bi. Michelle Nunn mara baada ya kufungua Mkutano wa Taasisi hiyo uliyofanyika Hyatt Regency Jijini Dar es salaam tarehe 13 Mei 2024. Kulia ni Mkurugenzi Mkaazi wa Taasisi ya Care Tanzania Bi. Prudence Masako.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa Taasisi ya Care International kushirikiana na kuiunga mkono Tanzania katika masuala ya mabadiliko ya tabianchi ikiwemo udhibiti na kukabiliana na maafa pamoja na kujenga uwezo wa mfumo wa tahadhari za mapema.


Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akifungua Mkutano wa Viongozi wa Kimataifa wa Taasisi ya Care International uliofanyika Hyatt Regency Jijini Dar es salaam. Amesema ushirikiano unaweza kuongezwa zaidi katika kujenga uwezo wa kustahimili mabadiliko ya tabianchi katika kuwezesha kilimo cha kisasa kinachoendana na hali ya hewa ili kuboresha tija na mavuno kwa wakulima wadogo.


 

Share To:

ASHRACK

Post A Comment: