Na Shomari Binda


MENEJA wa Wakala wa Wakala wa Barabara ( TANROADS) mkoa wa Mara Mhandisi Vedastus Maribe amepongezwa bungeni hii leo kutokana na usimamizi mzuri na madhubuti wa miradi ya barabara.


Pongezi hizo zimetolewa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara Ghati Chomete wakati akichangia bajeti ya Wizara ya ujenzi.


Kabla ya kutoa pongezi kwa meneja huyo mbunge Ghati alianza kutoa mchango wake kwa kumshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwaajili ya miradi ya mkoa wa Mara ikiwemo ya barabara za lami.


Amesema kutokana na miradi iliyopo licha ya fedha kuchelewa kufika kwa wakandarasi lakini usimamizi umekuwa mzuri kutoka kwa meneja wa mkoa.


Ghati amesema kazi inayofanywa na meneja huyo inapaswa kuungwa mkono na hata wabunge wa mkoa wa Mara watakubali kazi anayoifanya.


" Mheshimiwa Bashungwa nikupongeze pia kazi kubwa unayoifanya kwa kumsaidia Rais Samia lakini kwa mkoa wa Mara unaye msaidizi mzuri.


" Nimpongeze meneja mhandisi Vedastus Maribe na wasaidizi wake kwa kazi nzuri wanayoifanya katika usimamizi wa miradi iliyopo",amesema Ghati.


Amesema mradi wa Sanzati/Nata uliokuwa umekwama kwa kilometa 40 sasa umefikia 45 na kudai mkandarasi bado anadai zaidi ya bilioni 5.


Mbunge huyo amesema ipo miradi mingine ya Mogabili/Nyamongo na mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege inayosimamiwa na TANROADS Mara ambayo wakandarasi wanadai na kuomba walipwe kwa haraka ili kazi ziendelee.


Amesema licha ya mkandarasi kudai kwenye mradi wa uwanja wa ndege wapo wananchi wanaodai fidia ya zaidi ya bilioni 3 na kuomba pia wslipwe kwa kuwa wanaipenda serikali yao na ndio maana walipisha maeneo.

Share To:

ASHRACK

Post A Comment: