Na Shomari Binda
MBUNGE wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Muhongo amewaomba wabunge wakati wa majadiliano kuomba fedha kuongezwa kwenye bajeti ya Wizara ya ujenzi ifikie tilioni 3.5
Kauli hiyo ameitoa bungeni hii leo wakati akichangia kwenye bajeti ya Wizara hiyo katika bunge la bajeti linaloendele.
Kabla ya mchango wake kwenye Wizara hiyo Muhongo alianza kwa kumshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kwa asilimia 100 maombi ya Musoma vijiiini.
Amesema katika maombi hayo waliomba maombi ya masuala ya umwagiliaji na barabara na yote yamekubaliwa.
Muhongo amesema fedha za miradi kwenye bajeti hiyo in tilioni 1.69 ambapo ukitoa madeni inabaki bilioni 700 ambayo ukiigawa kutokana na maombi no fedha kidogo.
Amesema katika majadiliano amewaomba wabunge wapendekeze kiasi hicho cha tilioni 3.5 ili miradi iweze kutekelezwa vizuri.
Mbunge huyo amesema kuomba kuongezewa fedha sio jambo geni kufanyika ili kuweza kukamulisha ujitaji.
Amesema moja ya maeneo ambayo fedha zinapatikana ni pamoja na nje na kumshukuru Rais Samia namna anavyotoka katika kutafuta fedha.
Akizungumzia ujenzi wa barabara ya Musoma-Makojo hadi Busekera kilometa 92 amesema Wizara ya Ujenzi ipo kwenye matayarisho ya manunuzi (kumpata Mkandarasi) yanakamilishwa.
Amesema barabara litajengwa kwa awamu mbili kwa kuanza na km 40 ambapo kitabu cha bajeti ukurasa wa 116 unaorodhesha barabara hilo kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025.
Ukurasa wa 129 unaorodhesha daraja la Suguti kuwa moja ya madaraja makubwa yatakayojengwa mwaka wa fedha 2024/25
Ameongeza kuwa hadi leo ni kilomita 5 tu zimejengwa kwa kiwango cha lami kwenye barabara la Musoma-Makojo-Busekera huku serikali ikiendelea kusisitiza dhamira yake ya kujenga barabara lote kwa kiwango cha lami.
Post A Comment: