Mkuu wa mkoa wa Lindi mheshimiwa Zainab Telack akizindua mpango mkakati wa kuinua elimu ya msingi na sekondari katika mkoa wa Lindi
Mkuu wa mkoa wa Lindi mheshimiwa Zainab Telack akizindua mpango mkakati wa kuinua elimu ya msingi na sekondari katika mkoa wa Lindi
Mkuu wa mkoa wa Lindi mheshimiwa Zainab Telack akizindua mpango mkakati wa kuinua elimu ya msingi na sekondari katika mkoa wa Lindi
Fredy Mgunda, Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi umezindua mpango mkakati wa elimu ya msingi na Sekondari kwa mwaka 2024 kwa lengo la kuongeza ufaulu wa elimu kwa wanafunzi wanaosoma katika mkoa huo.
Akizungumza wakati wa sherehe za utoaji tuzo za elimu kwa wadau mbalimbali wa sekta ya elimu Mkuu wa mkoa wa Lindi Zainab Telack alisema kuwa wamezindua mpango mkakati wa elimu kwa lengo la kutatua changamoto 15 zilizopo katika elimu ya msingi na sekondari katika mkoa huo.
Telack alisema kuwa baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na hali ya ikama ya walimu wa Shule za Msingi na Sekondari na hali ya msawazo wa walimu, kutathmini hali ya viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia elimu, changamoto ya uwepo wa wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kwa darasa la kwanza na la pili, zoezi la utoaji wa chakula katika shule za msingi na Sekondari.
Alisema kuwa changamoto nyingine ni pamoja na mpango wa utoaji wa motisha kwa walimu, wanafunzi, wasimamizi wengine wa walimu, mpango wa uandaaji mitihani ya majaribio kwa watahiniwa wa mitihani ya kitaifa.
Mpango huu wa elimu kwa mwaka 2024 umezinduliwa na kukabidhiwa kwa viongozi wasimamizi wa elimu wa Mkoa na Wilaya ili kuhakikisha ufaulu unaendelea kuongezeka kwa ngazi zote za elimu sanjari na kuchochea maendeleo ya Sekta ya elimu kwa ujumla.
"Mpango Mkakati wa Elimu uliozinduliwa umejikita kutatua changamoto 15 ambazo ngazi ya elimu ya msingi na sekondari zinapaswa kuzisimamia kwa muda maalum uliopangwa" alisema Telack
Post A Comment: