MAKAMU wa Rais Dkt. Philip Mpango leo Mei 9 amezindua kampeni ya pili ya Mtu ni afya , yenye kauli Mbiu ya Afya yangu Wajibu wangu katika uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya Stendi ya zamani ya mabasi Mailimoja Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Katika uzinduzi huo Dkt. Mpango amewataka wananchi kujikinga na magonjwa ya Miripuko kwa kufuata maelekezo ya Wataalamu wa Afya pamoja na kuzingatia kanuni bora za usafi wa mazingira.
"Natoa wito kwa kuanzia ngazi ya serikali ya mtaa kote nchini wekeni mikakati ya kutunza mazingira,ujenzi wa mutaro ya maji taka ikiwa ni njia mojawapo yakutokomeza mazalia ya wadudu ambao husababisha magonjwa ya miripuko,pia kuweni na utamaduni wa kupima afya zenu sababu kinga ni bora kuliko tiba ambazo huleta gharama" amesema Dkt.Mpango.
"Takwimu zinaonesha kwamba kati ya wagonjwa 100,000 25 huumwa ugonjwa wa sukari na kati ya wagonjwa 100,000 huumwa ugonjwa wa Shinikizo la damu huku ugonjwa wa Kisukari ukiwa ni tishio kubwa na kusababisha wagonjwa wengi kufariki dunia" amesema Dkt.Mpango.
"Magonjwa yasiyoambukiza yanachangia vifo kwa asilimia 33 nchini huku historia inaonesha kuwa mwaka 1980 ilikuwa asilimia moja tu ya Watanzania waliokuwa wakisimbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu tofauti na ilivyo sasa ambapo ugonjwa wa Kisukari unaathiri kwa asilimia 25 huku ugonjwa wa shinikizo la damu unaathiri kwa asilimia tisa.
Aidha Dkt. Mpango amewataka wadau wakiwemo vyombo vya habari na wasanii kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kampeni hii ya pili inafanikiwa zaidi kwa kutoa elimu ya namna ya kupambana namagonjwa haya yasiyoambukiza kwa kupitia vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii huku kwa upande wa wasanii amewataka kutumia sanaa na ubunifu wao katika kusambaza elimu ya afya na umuhimu wa kufanya mazoezi kwani itawafikia wananchi moja kwa moja.
Dkt.Mpango amesisistiza ujenzi wa vyoo bora na kujiepusha kutupa taka ovyo kuanzia ngazi ya familia, kujenga tabia ya kunawa mikono kwa kutumia maji tiririka,kuchemsha maji ya kunywa kwa afya yao pia amehimiza hedhi salama kwa wanafunzi na usafi kwenye mazingira ya Shule, Halmashauri, Majiji na Wilaya ikiwa pamoja na kuacha tabia ya kutupa taka ngumu.
Makamu wa Rais ambaye ni mlezi wa Mkoa wa Pwani ametoa wito kwa Wizara ya Afya kwa kushirikiana na TAMISEMI kuziwezesha Idara za Afya katika Halmashauri za Wilaya,Manispaa,Miji na Majiji ili kuimarisha mifumo ya miundombinu na ufuatiliaji na utambuzi wa magonjwa ili iwe rahisi kukabiliana nayo pindi inaporipuka.
Kampeni Mtu ni Afya ilizinduliwa rasmi mwaka 1973 huku lengo likiwa ni kupambana na adui maradhi huku ikifuatiwa na kampeni zingine mbalimbali ikiwemo usichukulie poa Nyumba ni choo.
Naye Waziri Ummy amese makuwa kwa kupitia kampeni hii ya Mtu ni Afya awamu ya pili Benki ya Dunia imetoa bilioni 5.5 kwa ajili ya utekelezaji utakaotekelezwa kwa awamu kwa miaka saba.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amesema kuwa katika Mkoa umejidhatiti katika kudhibiti uharibifu wa mazingira ambapo kumekua na uendeshwaji wa Oparesheni mbalimbali za kuwadhibiti waharibifu wa mazingira hadi sasa wamekamata pikipiki 900 (Busta) zinazobeba mkaa kinyume na utaratibu na watuhumiwa 79 ambao nao upelelezi unaendelea na watafikishwa Mahakamani
Post A Comment: