Waraibu watatu wa dawa za kulevya wenye makazi yao jijini Arusha wameshiriki katika shindano la ‘Samia Challenge’. Shindano hilo ili uweze kuwa mshindi katı ya mshindi wa kwanza hadi watatu lilimtaka mwanachi wa Mkoa wa Arusha kushiriki katika kutaja na kuelezea miradi iliyotekelezwa au inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka mitatu tangu aingie madarakani, shindano hilo lilifanyika katika ukumbi wa Arusha Mall uliopo jijini Arusha.
Shindano hilo limefanyika tarehe 26.05.2024 jijini Arusha ambapo Mgeni rasmi katika shindano hilo la “Samia Challenge” alikuwa Mhe. Patrobas Paschal Katambi Mb, ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) ambaye alikaribishwa na mwenyeji wake Mhe. Felician Mtahengerwa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha. Zaidi ya watu 300 ambao wengi wao wakiwa vijana walipata fursa ya kuhudhuria shindano hilo.
Miongoni mwa washiriki ambao ni Waraibu waliweza kutaja miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kuongezeka kwa Vituo vya Huduma za Matibabu ya Uraibu na Utengamao nchi nzima. Mraibu mmoja katı ya watatu walioshiriki shindano hilo alifanikiwa kushinda zawadi ya kiasi cha shilingi elfu 50.
Ofisi ya DCEA Kanda ya Kaskazini itaendelea kutambua vipaji mbalimbali vya waraibu wa dawa za kulevya katika maeneo yao wanayoishi pamoja na kuwapatia fursa mbalimbali inayopatikana katika jamii.
Post A Comment: