Halmashauri ya Wilaya ya Rombo imefanya kikao cha Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe chini ya Mwenyekiti wake ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mh. Raymond Steven Mwangwala leo Mei 3 2024.
Katika Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa wilaya kilichowahusisha wajumbe mbalimbali ikiwemo Maafisa Watendaji wa Kata, wakuu wa Idara za ELIMU msingi na sekondari kimeazimia kuhakikisha shule zote katika Wilaya ya Rombo zinapanda mboga za majani ili kuboresha mlo kwa wanafunzi.
"Ninaagiza watendaji na maafisa elimu wakishirikiana na waalimu wakuu muhakikishe kila shule inakuwa na bustani ya mboga za majani kwajili ya kuboresha mlo wa mchana kwa wanafunzi na nitapita kukagua nijionee hata kama hakuna eneo zipo njia mbadala kama kupanda mboga kwenye mifuko na kadhalika hivyo sitaki visingizio" Mhe. Mwangala aliagiza.
Katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mh. Raymond Mwangwala pia amewasisitiza Maafisa Watendaji wa Kata kuwa, hadi ifikapo kikao kijacho watendaji wote wawe wamekwisha kuwasilisha maoni ya sheria za ndogo za lishe za vijiji na kata kwa mwanasheria wa halmashauri kwaajili ya kufanyia kazi.
Mkuu wa Wilaya Pia alipata wasaaa wa kupongeza jitihada za wataalamu na viongozi kwa kuendelea kutoa elimu ya lishe bora kwa jamii kwani matokeo chanya yameonekana katika taarifa iliyowasilisha na Bibi lishe na kuomba zaidi ushirikiano katika kutatua changamoto chache zilizobakia ili kufikia malengo kwa asilimja 100%.
Nae Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo Bi. Philiberta Rogath wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya tathmini ya lishe, alitilia msisitizo juu ya Lengo la mkataba wa lishe kuwa ni, kuhakikisha jamii inapata lishe bora na kuondoa kabisa tatizo la utapiamlo.
Zaidi sana Bibi lishe amewaomba watendaji wa kata na vijijji kipindi watoapo elimu za lishe wahakikishe wanapiga picha za matukio kama ushaidi na kuziwasilisha wawasilishapo taarifa za utekelezaji wa mkataba wa lishe katika eneo husika ili kupunguza maswali na kuonesha kuwa kweli utekelezaji unafanyika kwa vitendo.
Post A Comment: