Mkuu wa Wilaya ya llala Mhe. Edward Mpogolo amefungua warsha ya siku mbili(2) ya Uhuishaji wa Mpango Mkakati pamoja na Mpango kabambe wa Halmashauri iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa APC Hotel- Bunju na kuhudhuli wa na Viongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya pamoja na Watumishi wa Jiji la DSM.

Akiongea wakati wa ufunguzi, Edward Mpogolo amesema baada ya warsha hiyo anataraji kuona ubunifu mpya wakubuni vyanzo vipya vya mapato,kuimarisha mikakati na mbinu za kukusanya mapato, kulinda mapato yanayopatikana pamoja na kusisitiza mahusiano na ushirikiano kazini.

Mada zilizowasilishwa ni pamoja na afya ya akili na magonjwa yasiyo ambukizwa, Usimamizi wa Miradi, Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato, Usimamizi wa Ujibuji wa Hoja za Ukaguzi kutoka kwa Mkaguzi wa Hesabu za Serikali(CAG)pamoja na Mkaguzi wa Ndani, Mdahalo juu ya Ilala bora pamoja na Usimamizi wa Serikali za Mitaa na Utawala Bora..







Share To:

Post A Comment: