Waziri wa Madini Mh Anthony Peter Mavunde amewataka Watumishi wa Wizara ya Madini kuacha kufikiri ndani ya boksi badala yake wawaze nje ya boksi kwa kuleta vitu tofauti ili kukuza Wizara kwa kuleta Ubunifu na Kushauriana na Waziri.


Waziri Mavunde ameyasema hayo mapema Leo hii Jijini Dodoma katika ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Madini la kujadili na kupitisha Bajeti ya Wizara.

Aidha ameongeza kuwa watu waache kufikiri vitu vilevile kila siku waje kivingine ili kuleta makurdi yaliyotarajiwa.

"Niwaombe kila mtu aliyemo humu ndani acheni kufikiri ndani ya boksi,fikiri nje ya boksi,mje na vitu tofauti,mmekuwepo hapa kwa muda mrefu sana hivyo tusiendelee kufikiri vilevile tuje na vitu tofauti vya kukuza Wizara yetu hii mwisho wa siku tulete makusudi yaliyotarajiwa".

"Mimi tangu nimeingia Wizara ya Madini ni mtu mmoja tu aliyewahi kunigongea mlango na kuja kunipa ushauri,wengine kwanini hamji, Wizara hii sio ya kwangu,Wizara ni yetu sote mimi nimepewa kipande tu cha kusimamia Sera na Sheria lakini Injini ni ninyi na ninyi mna uwezo mkubwa kuliko tuliokaa mbele. Mna ushauri mna ubunifu njooni tushaurianae Wizara ya kwetu hii".

Sambamba na hayo Waziri Mavunde amewataka wakuu wa Idara na Vitengo wenye Miradi ya maendeleo ndani ya sekta ya Madini kutumia fedha za Bajeti ya Wizara kwa wakati na kwa matumizi sahihi ili zisirudi Hazina na kuacha miradi ukiwa haijakamilika na atakayesababisha fedha kurudi Hazina basi atarudi nazo.

"Yaani Mkuu yeyote wa Idara au Kitengo ambaye Ana mradi halafu eti fedha zikarudi Hazina atakwenda nazo kwasababu sisii tunapambana kuleta fedha ndani ya wizara halafu ninyi hamtumii tutakuwa tunapoteza muda tu,Kwahiyo niwaombe kupitia kikao hiki mkae mzungumze vizuri me na mikakati ya matumizi sahihi ya fedha hizi za maendeleo ili mwisho wa siku ziweze kuleta tija kwa Taifa letu la Tanzania ".

"Shida yetu ni kwamba Wizara ya Madini ndio tunaongoza kwa kutokutumia fedha kwa wakati. Niliwatangazia na ninarudia tena kusema moja kati ya jambo ambalo litamfanya mtu asiwepo kwenye nafasi yake ni kushindwa kutumia fedha kwa wakati,nitamuondoa ampishe mtu mwingine yani watu wanatafuta fedha sisi hatuzitumii kwa wakati,Bajeti yetu ni ndogo sana na hili katika kikao chenu mtajadiliana pia nilishawaelekeza ili tuwe tuwe tunafanya fedha zunatumika ndani ya muda,atakayesababisha fedha kurudi Hazina kwangu na yeye pia aende nazo, fedha zitumike ndani ya muda na kwa matumizi ya maendeleo tu na si vinginevyo".

Akisoma Taarifa ya Baraza hilo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Baraza Bwana Msafiri Mbibo amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 wizar6imejiwekea vipaumbele vyake ikiwemo kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli na kuendeleza madini muhimu na mkakati.

"Ili kuhakikisha sekta ya madini inakuwa na kuendelea kuwanufaisha Watanzania ikiwa ni pamoja na kukuza mchango wa sekta ya Madini kwenye pato la Taifa,katika mwaka wa fedha 2023/2024 Wizara imejiwekea vipaumbele ikiwemo ukusanyaji wa maduhuli na kuongeza mchango wa sekta ya Madini kwenye pato la Taifa,kuendeleza Madini muhimu na Madini Mkakati,kuendeleza na kusogeza huduma za ugani kwa Wachimbaji wadogo,kuhamasisha shughuli za uongezaji thamani Madini,kuhamasisha uwekezaji na Biashara katika sekta ya Madini na uanzishwaji wa Minada na maonesho ya Madini ya Vito na mwisho kuzijengea uwezo Taasisi zilizo chini ya Wizara ili ziweze kufanya majukumu yake kwa ufanisi zaidi".

Naye Afisa Kazi Mkoa wa Dodoma Bi Eunice Tesha ametumia nafasi hii kuwakumbusha wajumbe wa Baraza waliochaliwa kutosahau kutumia nafasi hii kuwakilisha na kutoa maoni kama ilivyo umuhimu wa Baraza.

Awali akitoa salamu kutoka chama cha wafanyakazi TUGHE Bwana Joseph Ngulumwa ambaye ni Mwenyekiti Tughe Tawi la Madini amesema kuwa anatambua kuwa viongozi wa Wizara wanaendelea kutekeleza Sera ya Madini ikiongozwa na kauli mbiu ya Vision 2030,Madini ni Maisha na Utajili,inayolenga kugundua hazina zaidi za Madini ili kuapata wawekezaji wenye tija.

"Mheshimiwa Mwenyekiti,Tunatambua kuwa viongozi weru wa Wizara wanaendelea kutekeleza Sera ya Madini ikiongozwa na kauli mbiu ya Vision 2030,Madini ni Maisha na Utajiri inayolenga kugundua hazina zaidi ya Madini katika maeneo mengi yatayosaidia nchi kupata wawekezaji kwa tija zaidi.

Baraza hili linafanyika ikiwa ni Mahsusi kupitia,kujadili na kupitisha Bajeti ya Wizara na miezi miwilo iliyopita Mkutano wa Baraza la Tathmini ulifanyika kuona utekelezaji wa Mipango ya Wizara.



Share To:

Post A Comment: