Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Komredi Jokate Urban Mwegelo (MNEC) amesema Viongozi Wakuu wa Chama Cha Mapinduzi Wana Imani kubwa na Vijana hivyo Vijana wana Kila  Sababu ya Kufanya kazi kwa bidii kulilinda Imani hiyo.

"Sisi wote ni Mashahidi wa mambo makubwa yanayofanywa na Viongozi wetu na kama mtakumbuka Juzi tarehe 26 Aprili tumetoka kusherekea Sherehe za Miaka Sitini (60) ya Muungano wetu kwa namna ya kipekee sana na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hotuba yake aliyoitoa kwa Wananchi alionyesha ni kwa kiasi gani Vijana ndio nguvu kazi ya Taifa kutokana na Wingi wetu"

"Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali yetu ya Mapinduzi ya Zanzibar zimewekeza kubwa kwa Vijana wote wa Kitanzania na Viongozi wetu Wakuu wana Imani kubwa na sisi Vijana katika ujenzi wa Taifa letu, Hivyo tuna wajibu wa Kuilinda Imani hii Kubwa lakini pia kuulinda Muungano wetu kwa wivu mkubwa sana". Alisema Komredi Jokate.








Share To:

Post A Comment: