Viongozi Wakuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa wakiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Komredi Mohammed Ali Kawaida (MCC) wamewasili Rufiji mkoani Pwani kutoa faraja na kuwajulia hali wananachi wa Rufiji kutokana na athari za Mafuriko yaliyojitokeza kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.

Viongozi wa Umoja wa Vijana walioambatana na Mwenyekiti Komredi Kawaida ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Rehema Sombi Omary (MNEC), Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Jokate Urban Mwegelo (MNEC) na Maafisa wa UVCCM Makao Makuu.

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umewasilisha Mahitaji ya Chakula ikiwemo Mchele, Mafuta na Sukari.

Mafuriko ya namna hii yalitokea mwaka 1968,1972,1978,1998,2020 na mwaka 2024 Mafuriko yalianza 5 Machi ambapo yamesababisha Kaya 23670 kuathirika na mafuriko ya sasa na wahanga wa mafuriko Wamehifadhiwa katika makambi manne yaliyoandaliwa na Serikali na baadhi wameenda kwa ndugu jamaa na marafiki.











Share To:

Post A Comment: