Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ikiongizwa na Mwenyekiti wake Ndugu Mohammed Ali Kawaida (MCC) wamekabidhi msaada wa Chakula kwa wananchi wa Rufiji walioathirika na mafuriko katika maeneo hayo.
Ndugu Kawaida ameelekeza Viongozi wa Rufiji kuhakikisha misaada yote inayotolewa inawafikia wananchi hao waliothirika na Mafuriko
"Niwasihi sana viongozi hakikisheni misaada hii inawafikia walengwa ambao ni wananchi wenzetu walioathirika na mafuriko na tuendelee kuwa faraja kwa ndugu zetu" Alisema Kawaida
Aidha Ndugu Kawaida amewahakikishia wananchi wa Rufiji kuwa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi itaendelea kuwa karibu nao katika kipindi hiki kigumu wanachopitia kwani ni Utamaduni wa UVCCM kuwakimbilia Wananchi pale wanapopatwa na Matatizo.
"Ndugu zangu sisi Jumuiya ya Vijana tuna utamaduni wetu wa kuishi kama ndugu wamoja ndio maana kauli Mbiu yetu ni "Kulinda na Kujenga Ujamaa", Hivyo niwahakikishie kuwa tutaendelea kuwa karibu na ninyi katika kipindi hiki kigumu"
Mwisho Ndugu Kawaida amewasihi Watanzania na Wadau mbalimbali wawakimbilie Wananchi wa Rufiji kuwasaidia wananchi wa Rufiji na sio kufanya Siasa.
Post A Comment: